Msichana mwenye umri wa miaka miwili huko nchini Marekani anahitaji kuchangiwa damu mara kadhaa ili kukabiliana na ugonjwa wa saratani.
Hali yake imegusa nyonyo za watu wengi, kampeni ya kuwatafuta wachangiaji damu inayofanana na ya mtoto huyo.
Zainab Mughal ni mtoto mwenye damu ya aina ya kipekee duniani ambayo inampa wakati mgumu kupata matibabu ya ugonjwa wake.
Waratibu wa kampeni hiyo wanasema zaidi ya watu 1,000 wamefanyiwa majaribu , lakini mpaka sasa ni watu watatu pekee ndio wenye damu inayohitajika .
Madaktari wanasema bado watahitajika wachangiaji kati ya saba hadi 10 ili kuweza kumtibu saratani yake .
Mapema mwaka huu Zainab aligundulika kuwa na saratani ya 'neuroblastoma', ambayo hujitokeza mara chache na kuathiri zaidi watoto .
Aidha kwa mujibu wa kituo cha damu 'Oneblood' kimebainisha kuwa uhamisho wa damu utahitajika kwa kipindi chote cha matibabu yake, lakini damu ya Zainab ni "nadra sana" kupatikana kwa sababu imekosa vimelea vya kundi 'B' ambavyo watu wengi huwa navyo katika seli zao za damu nyekundu.
Pia imebainika kuwa wachangiaji damu ambao wataweza kuendana na damu yake ni watu wenye asili ya Wapakistan ,Wahindi ama Wairan ambao wana aina ya damu ya kundi O na A.
Lakini hata katika idadi fulani ya watu wa Marekani , chini ya asilimia 4 hukosa vimelea hivyo vya kundi B.
Hata hivyo mwili wa Zainab utakataa damu yoyote ambayo itakuwa haijakidhi viwango vyote.
Wachangia damu wawili wenye damu zinazoendana naye tayari wamekwisha patikana nchini Marekani, ambapo mwingine mmoja amepatikana nchini Uingereza.
Kiongozi wa maabara katika kituo cha OneBlood, Frieda Bright, ameshangazwa sana kwani amekuwepo kwa miaka ishirini kwenye taaluma hii lakini hii ni mara ya kwanza kujitokeza kwa tatizo kama hilo.
Kituo hiko cha asasi isiyokuwa ya kiserikali, OneBlood hufanya kazi na mabenki mengine ya damu pamoja na Programu ya kutafuta wachangiaji damu Marekani 'ARDP'ambayo husaidia zaidi kupata wachangiaji wenye damu za kipekee duniani.
"Licha ya kuwa damu haitamponya lakini ni muhimu sana kuipata ili apate matibabu ya saratani, "Bi Bright amesisitiza katika video ya kampeni hiyo.
Baba yake Zainab ,Raheel Mughal alisema kuwa binti yake aligundulika na ugonjwa huo mwezi Septemba mwaka huu.
Anasema walilia sana kwani jambo hilo hawakuwahi kutarajia kama litatokea.
Yeye na mama wa mtoto huyo walijitolea kutoa mchango wa damu zao wenyewe lakini madaktari waligundua kuwa hakuna hata mmoja ambaye ana damu inayoendana na ya Zainab.
Walitafuta watu wengi katika familia yao bila mafanikio na walipoenda kuchangisha damu kwa watu wengi zaidi ndio watu wakawa na taarifa zaidi .
Kwa mujibu wa kituo cha OneBlood wanasema matibabu ya kutumia mfumo wa mionzi tayari imekwisha kupunguza ukubwa wa tatizo la saratani.
"Maisha ya binti yangu yanategemea damu.
Nimeshangazwa sana na jinsi wachangiaji damu wanavyoangaika kuokoa maisha ya binti yangu na kwa kazi wanayofanya sitoweza kuwasahau daima", Mughal alisema
Comments
Post a Comment
Here