Skip to main content

Posts

Showing posts with the label AFRIKA MASHARIKI

ATM za maziwa yawakomboa wafugaji wa Kilimanjaro.

Maziwa ,kilimanjaro Nchini Tanzania wengi wao wanaposikia ATM kitu cha kwanza wanachoweza kufikiri huenda ikawa ni chombo cha kutolea fedha. Jambo ambalo ni tofauti huko Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro ipo ATM ya kwanza ya maziwa ambayo imeguka kivutio kwa wakazi wa mkoa huo. Unaweza ukajiuliza ATM hiyo inafanyaje kazi? Nancy Manase ni wenyekiti wa umoja wa wanawake wa maziwa ''Uone labda tulikuwa tunauza lita mia tatu kwa siku au mia nne sasa tumeongezea lita mia moja juu kwahiyo ni faida na msimu huu ni ule msimu unaokuwa na maziwa mengi sana huku kwetu maziwa yanakuwa mengi mpaka yanamwagwa kwahiyo mpaka sasa hivi hatujamwaga maziwa''. ATM inatusaidia na watu wamepata elimu kunywa maziwa ni afya kwa sababu hata usipokula kitu kingine inakutosha'' Kila lita moja inagharimu wastani wa dola moja Lakini katika mashine...

Hoteli ya DusitD2 Nairobi: Washukiwa watano wa shambulio la Dusit wawasilishwa mahakamani wakificha nyuso zao

Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani . Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada. Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea. Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 . Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao. Ni washukiwa wa kwanza kuwasilishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2 . Lakini hawakusomewa mashtaka yao. Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa. Washukiwa wanne ni raia wa Kenya huku wa tano akiwa raia wa Canada mwenye mizizi ya Kisomali., Mapema maafisa wa polisi waliambia BBC waliwakamata watu saba. Mtu mmoja ambaye alionekana na washukiwa hao kabla ya shambulio anaaminika kuwa miongoni mwa wale waliozuiliwa lakini hakuwasilishwa ma...

Burundi: Rais Pierre Nkurunziza asema Rwanda imekuwa adui, ataka kikao cha EAC kiandaliwe

Image caption Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuna mzozo wa wazi kati ya taifa lake na taifa jirani na Rwanda katika kinachoonekana kuwa kudorora zaidi kwa uhusiano baina ya mataifa hayo mawili. Rwanda na Burundi zimekuwa na uhasama kwa muda sasa, Burundi ikiituhumu Rwanda kwa kuhusika katika jaribio la kupindua serikali mwaka 2015 ambalo lilifeli. Burundi hudai kwamba Rwanda iliwafadhili waliohusika na kwamba inatoa hifadhi kwao. Rwanda mara kwa mara imekuwa ikikanusha tuhuma hizo. Rais Nkurunziza amemwandikia barua mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Yoweri Museveni ambaye ni rais wa Uganda akisema Rwanda sasa si mshirika tena ndani ya jumuiya bali ni kama adui. "Rwanda ndiyo nchi pekee katika kanda hii ambayo ndiyo moja wa wahusika wakuu katika kuvuruga uthabiti wa taifa langu na kwa hivyo siichukulii kama taifa mshirika, lakini kama adui ya nchi yangu," barua hiyo, ambayo inaonesha ilitiwa saini na Bw Nkurunziza t...