Skip to main content

Posts

Showing posts with the label AFYA

Fahamu ukweli wa dhana tano kuu kuhusu nyoka na maadhimisho ya nyoka duniani

Huku Tarehe 16 mwezi Juni ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya nyoka duniani mnyama huyo hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika. Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani. Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika. Uso kwa uso na nyoka hatari Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya. Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu. Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. Hebu tuwafahamu zaidi. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES ...

VYAKULA 10 VINAVYOFAA KWA WANAUME.

1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito. 2. Samaki kutoka baharini, asa wenye magamba ambao huwa na virutubisho vya zinc vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu za kiume. Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kuku huwa na kiasi kikubwa cha madini haya. 3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia kuondoa mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya moyo. 4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia. 5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo husaidia kujenga  misuli imara. Pia ina bacteria rafiki wanaosaidia kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo. 6. Ndizi mbivu, Ina virutubisho vya potassium ambavyo uimarisha misuli, mifupa na kupunguza ...

Je unayafahamu maeneo muhimu ya kuyasafisha nyumbani kwako?

When preparing raw food, surfaces have to be cleaned thoroughly afterwards.         Watu wanapaswa kufahamu namna ya kuzuia viini vinvayosababisha magonjwa vinavyosambaa nyumbani kliko kufanya usafi wa maeneo wanayoyaona kuwa ni "machafu", kwa mujibu wa ripoti ya British Royal Society for Public Health (RSPH). Kuosha mikono, nguo na kusafisha sehemu kwa wakati muafaka ndio chanzo cha afya nzuri- lakini mtu mmoja kati ya wanne wanadhani hilo sio muhimu, ripoti hiyo inaonya. Kulifanya hilo kwa njia sawa kunaweza kupunguza maambukizi na magonjwa kukaidi dawa za antibiotic. Na hakuna usafi 'unaopita kiasi'. Kuna mchanganyiko kwa umma kuhusu utofuati katiya uchafu na viini vya uchafu au germs, usafina afya. Katika utafiti wa watu 2,000, asilimia 23 walidhani watoto wanihatji kushika uchafu ili kujenga mfumo wa kinga mwilini. Lakini wataalamu katika ripotihiyo wanasema "kuna uwezekano wa madhara" yanayoweza kuwafanya kupata maambukizi ...

Samaki wa Mexico walio na uwezo wa kurekebisha matatizo ya moyo

Haki miliki ya picha BHF Image caption Samaki wa tetra anayeishi katika mito kaskazini mwa Mexico wanaweza kuponya mioyo yao Samaki anayeweza kuurekebisha moyo wake huenda ndio suluhu ya matibabu kwa watu wenye matatizo ya moyo, kwa mujibu wa utafiti. Wanasayansi wanao wachunguza samaki wa Tetra kutoka nchini Mexico wamegundua maeneo matatu ya mfumo wa samaki huyo uliochangia uwezo wake kuunda upya tishu za ndani ya moyo. Jeni moja imeonekana kuwa na jukumu kuu katika mfumo huo. Watafiti wanatumai  utafiti  wao siku moja utafanikisha uponyaji wa misuli ya ndani ya moyo kwa wagonjwa ambao wamewahi kupata mshtuko wa moyo. Maelfu ya watu huishi na matatizo ya moyo baada ya kupata mshtuko wa moyo. Kwasababu binaadamu hawawezi kuunda upya msuli ulioharibika, au kujeruhiwa kwa moyo, na mara nyingi watu hulazimika kuishi na hali hiyo au kuishia kufanyiwa upandikizaji wa moyo. Dalili za samaki kwenye pango Kwa utaifiti huu, uliofadhiliwa na taasisi ya British Heart Foun...

‘Wanawake wanaoamka mapema wapo kwenye uwezekano mdogo kupata saratani ya matiti

Wanawake wanaoamka mapema wapo katika uwezekano mdogo wa kupata saratani ya matiti, kwa mujibu wa watafiti nchini Uingereza. Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Briton wanasema sababu ya uhusiano wa muda wa kuamka na hatari ya saratani bado inahitaji kufahamika. Wanaongeza kuwa ugunduzi huo ni muhimu kwa kuwa kuwa unamuathiri mwanamke. Saa ya mwili Kila mtu ana kile kinachofahamika kama saa ya mwili ambayo inaonyesha jinsi mwili unafanya kwa saa 24. Hi inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama circadian rhythm. Inaathiri kila kitu kutokana muda tunaolala, hisia zetu na hata hatari yetu ya kupatwa na mshutuko wa moyo. Lakini sio kila saa ya mwili ya kila mtu inayoonyesha muda ulio sawa. Watu wa asubuhi au "larks" huamka mapema, hufanya kazi mapema na huchoka mapema. Watu wa jioni au "owls" huwa na wakati mgumu kuamka mapema, huwa wa mazao baadaye jioni na hupenda kulala wakiwa wamechelewa. Hili huwa na athari kwa ugonjwa wa saratani? Watafii ...

MAYAI NA UMUHIMU WAKE

Kula yai kwa siku kunaweza kuwasaidia watoto wadogo wenye utapiamlo kuongeza urefu kulingana na utafiti wa miezi sita huko Ecuador. Haijalishi ikiwa ni yale yaliyo chemshwa, au ya kukaanga, na watafiti wanasema ni njia isiyo ghali ya kuzuia kudumaa. Miaka miwili ya kwanza maishani ni ya muhimu sana kwa ukuaji na maendeleo na kudumaa kunaweza kuleta madhara makubwa. Lishe duni ni sababu kubwa ya kudumaa, pamoja na maambukizi ya utotoni na magonjwa. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, WHO, watoto milioni 155 chini ya umri wa miaka mitano wamedumaa (wafupi kwa umri wao). Wengi wao wanaishi katika nchi zilizo na mapato ya chini na ya kati na wataalamu wa afya wamekuwa wakitafuta njia za kukabiliana na suala hilo. Lora Iannotti na wenzake walifanya majaribio katika nyanda za vijijini ya Ecuador na kuwapa watoto wadogo sana (wenye umri wa miezi sita hadi tisa) mayai, ili kuona kama yataweza kuwasaidia. Nusu tu kati ya watoto 160 ambao walishiriki katika majaribio wali...