Skip to main content

Posts

Showing posts with the label MICHEZO

As Roma kuzungumza na Waswahili kupitia Twitter

Haki miliki ya picha AS Roma Klabu ya mpira ya 'As Roma' nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza kutoka barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter. Kurasa hiyo ya As Roma itakuwa ikiandika habari zake kwa lugha adhimu ya kiswahili. Ukurasa huo wa lugha ya kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanatumia lugha ya kiswahili.  Akaunti hiyo ya Twitter imezinduliwa siku ya jumatano kwa video yenye maneno ya utani ya kiswahili. Akaunti hiyo imepokelewa vizuri na wasomaji wa kiswahili wa Tanzania na Kenya. Hakimiliki ya Picha @ASRomaSwahili @ASRomaSwahili Wengi wakiona kuwa ni ubunifu mzuri ambao unaonesha kuwajali mashabiki wanao...

Floyd Mayweather ampiga 'knockout' mara tatu Tenshin Nasukawa na kushinda katika raundi ya kwanza

Haki miliki ya picha AFP Image caption Mayweather aikuwa akitabasamu alipombwaga mpinzani wake Nasukawa Floyd Mayweather alihitaji sekunde 140 pekee kumshinda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa katika pigano la maonyesho lililokuwa na thamani ya dola $9m. Bingwa huyo mara tano wa zamani Mayweather mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo la muda mfupi mjini Tokyo alipombwaga mara tatu mpinzani wake mwenye umri wa miaka 20. Pigano hilo la raundi tatu lilimalizika huku Nasukawa akibubujikwa na machozi baada ya kikosi chake kurusha kitambaa cheupe ndani ya ulingo kikitaka pigano kusitishwa. Licha ya kurudi katika pigano hilo Mayweather alisema yeye amestaafu ndondi za kulipwa. ''Ni hatua ya kuburudisha tu, tulifurahia sana , alisema raia huyo wa Marekani ambaye alimshinda bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano la masumbwi mnamo mwezi Agosti 2017. ''Walitaka pigano hili kufanyika nchini Japan hivyobasi nikasema kwa nini lisifanyi...

Mbwana Ally Samatta: Nyota wa Tanzania amfunga kipa wa Liverpool aliyekumbwa na mkosi Europa League Besiktas v KRC Genk

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta aliendelea kutikisa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kwa kufungia klabu yake mabao mawili katika mechi iliyochezwa Alhamisi. Aliisaidia klabu yake ya KRC Genk kuwalaza Besiktas wa Uturuki kwa mabao 4-2. Katika mechi hiyo, langoni alikuwa kipa wa Liverool Loris Karius ambaye anakumbukwa kwa kufanya makosa makubwa na kuchangia Liverpool kushindwa kwenye fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei mwaka huu. Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya 23 na kisha akaongeza la pili dakika ya 70 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Joakim Maehle nyakati zote mbili. Mabao yote mawili aliyafunga kwa mguu wake wa kulia. Sababu ya Samatta kung’ang’aniwa England Mohamed Salah atuma ujumbe kwa kipa Karius Kipa wa Liverpool Loris Karius ashauriwa ahame Kipa wa Liverpool Loris Karius atishiwa maisha Besiktas walikomboa bao moja dakika ya 74 kupitia Vagner Loveawazisha dakika ya 74, lakini Genk waka...