Skip to main content

Posts

Showing posts with the label KITAIFA

ATM za maziwa yawakomboa wafugaji wa Kilimanjaro.

Maziwa ,kilimanjaro Nchini Tanzania wengi wao wanaposikia ATM kitu cha kwanza wanachoweza kufikiri huenda ikawa ni chombo cha kutolea fedha. Jambo ambalo ni tofauti huko Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa Kilimanjaro ipo ATM ya kwanza ya maziwa ambayo imeguka kivutio kwa wakazi wa mkoa huo. Unaweza ukajiuliza ATM hiyo inafanyaje kazi? Nancy Manase ni wenyekiti wa umoja wa wanawake wa maziwa ''Uone labda tulikuwa tunauza lita mia tatu kwa siku au mia nne sasa tumeongezea lita mia moja juu kwahiyo ni faida na msimu huu ni ule msimu unaokuwa na maziwa mengi sana huku kwetu maziwa yanakuwa mengi mpaka yanamwagwa kwahiyo mpaka sasa hivi hatujamwaga maziwa''. ATM inatusaidia na watu wamepata elimu kunywa maziwa ni afya kwa sababu hata usipokula kitu kingine inakutosha'' Kila lita moja inagharimu wastani wa dola moja Lakini katika mashine...

Bajeti 2019: Tanzania na Uganda zapendekeza kodi kwa mawigi na visodo

                           Waziri wa fedha Tanzania' ametangaza kodi ya 25% kwa uingizaji wa nywele zote bandia maarufu mawigi na 10% kwa zinazotengenezwa nchini katika jitihada za kukuza uchumi wa nchi. Waziri Philip Mpango ametangaza hatua hizo, ambazo zitaidhinishwa mwanzoni mwa mwezi ujao kama sehemu ya bajeti iliyosomwa jana, ya mwaka 2019 na 2020. Kadhalika kodi kwa visodo imerudishwa kutokana na kwamba hatua ya kuondoshwa kodi mwaka jana kwa bidhaa hizo muhimu kwa wanawake, haikusaidia kushuka kwa bei. Na badala yake Mpango ameeleza kuwa ni wafanya biashara wanaofaidi kutokana na kuondolewa kwa kodi hiyo. wanawake wengi huvaa nywele hizo bandia ambazo kwa wingi husafirishwa kutoka mataifa ya nje. Kwa makadirio, wigi hugharimu kati ya $4 na hata zaidi ya $130. Nchi ya Uganda, pia imeidhinisha kodi kwa mawigi, ndevu band...

Edward Moringe Sokoine MEMORIAL and PERSONALITIES

Edward Sokoine Edward Moringe Sokoine (1 August 1938 – 12 April 1984) was a two-term prime minister of Tanzania serving from 13 February 1977 to 7 November 1980 and again from 24 February 1983 to 12 April 1984. Edward Moringe Sokoine had a developmental conception of the village. Sokoine saw the village as a harbinger of self-reliant, national development and the peasant as an agency of change. He was a person of unimpeachable personal integrity. Edward Sokoine 2nd Prime Minister In office 13 February 1977 – 7 November 1980 President Julius Nyerere Preceded by Rashid Kawawa Succeeded by Cleopa Msuya In office 23 February 1983 – 12 April 1984 Preceded by Cleopa Msuya Succeeded by Salim Ahmed Salim Personal details Born 1 August 1938 Monduli, Tanganyika Died 12 April 1984 (aged 45) Nationality Tanzanian Political party CCM Other political affiliations Tanganyika Africa Nation Union Life and career In 1938, Sokoine was born in M...

Magufuli amtaka waziri 'avute bangi'

Image caption Rais wa Tanzania, Dokta John Magufuli ameonyesha kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi ya maji Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemtaka waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kuwa mkali kusimamia miradi ambayo imekusudiwa na serikali. Alipokua kwenye ziara ya kikazi mkoani Njombe, nyanda za juu kusini mwa Tanzania Rais Magufuli amekagua miradi mbali mbali ikiwemo kufungua barabara ya Mafinga mpaka Igawa yenye umbali wa kilometa 138.7. Kando na hilo Magufuli ameonyesha kutoridhishwa na utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya maji nchini Tanzania. Magufuli kwa lugha ya utani alimtaka waziri wa Maji Prof Mbarawa kuvuta bangi ili kuwa mkali. Amesema katika uhakiki wa miradi ya maji kuanzia mwaka 2013 mpaka 2018 palikua na miradi ya maji iliyohakikiwa na wataalamu kutoka wizara ya fedha ambapo kulikua na miradi ya thamani bilioni 119 miradi ya kweli ilikua na thamani ya bilioni 17. Kati ya bilioni 119 madai ya kweli ya mradi uliofanyika ni bilion...

Vijana wanavyokabiliana na 'uhaba' wa kondomu Zanzibar

Mashirika ya kijamii yamekuwa mstari wa mbele katika kampeni mbalimbali za kuhamasisha matumizi ya mipira ya kondom ili kuzua maambukiza ya magonjwa ya zinaa. Lakini katika baadhi ya maeneo visiwani Zanzibar matumizi ya kondomu si jambo la kawaida. Kondomu haiuzwi katika maduka ya kawaida, jambo ambao limekua likiwaumisha vichwa wanaharakati wa chama cha watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi visiwani humo. Kwa mujibu wa Wizara ya afya Zanzibar, maambukizi ya virusi vya Ukimwi yapo chini ya 1% lakini kwa upande wa makundi hatarishi kama vile watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi na pamoja na wanawake wanaofanya biashara ya ngono bado maambukizi ni makubwa. BBC imebaini kuwa changamoto kuu ni upatikanaji wa mipira ya kondomu hasa katika maduka ya kawaida. ''Ishawahi kunitokea'' ,anasema mmoja wa wanawake wanaofanya biashara ya ngono. ''Nataka kondomu lakini sehemu ya kupata hamna, inabi...

Fastjet: Shirika la ndege lapewa makataa kujieleza kwa nini wasifungiwe Tanzania

Shirika la ndege la Fastjet Airlines Limited maarufu kama Fastjet Tanzania limepewa makataa ya siku 28 kueleza sababu zinazoweza kuzuialisifungiwe kuendelea kuhudu Tanzania. Kwa mijibu wa Mamlaka ya Safari za Anga Tanzania, shirika la ndege la Fastjet limekosa sifa ya leseni ya usafiri wa anga kwa sababu halina ndege zozote kwa sasa. TCAA imesema ilitoa notice ya siku 28 ya kulitaka shirika hilo lisitishe mauzo kwa abiria. Na limeamuru shirika hilo kurejesha pesa kwa abiria hao au kuwatafutia usafiri katika mashirika mengine. Mamlaka hiyo pia imeamuru waliopata hasara wafidiwe kwa mujibu wa sheria, na watoe mpango mkakati kwa nini wasifutiwe leseni ndani ya siku 28, pia ikitokea shirika hilo limefungwa basi walipe stahiki za wafanyakazi. Fastjet tayari wametangaza kusitisha safari zake zote za mwezi Desemba na mwezi Januari. Na wameahidi kurejesha nauli za abiria wote kuanzia tarehe 20 mwezi de...

Uchaguzi 2020: Membe kufuata nyayo za 'hasimu' wake Lowassa?

Magufuli (kushoto) na Membe (kulia) walikuwa ni miongoni mwa makada wa CCM waliochuana kuwania tiketi ya urais. Je mchuano huo utarudiwa tena 2020? Jina la Bernard Camilius Membe ambaye amewahi kuwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 8 katika serikali ya Jakaya Kikwete limekuwa likigonga vichwa vya habari nchini Tanzania. Hali hiyo imetokana na kutuhumiwa na uongozi wa chama chake cha CCM kuwa na mikakati ya chinichini kumhujumu Rais wa sasa John Magufuli pamoja na kujiandaa kugombea urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020. Tuhuma zilizotolewa na Katibu Mkuu CCM, Dkt. Bashiru Ally kuwa Membe amekuwa na mwenendo wa kutia shaka ndani ya chama hicho na kumtaka afike ofisi za chama hicho jijini Dar es salaam kujitetea na tuhuma zinazomkabili. Siku chache baadaye Membe alijitokeza na kutoa taarifa kupitia kundi sogozi ambalo mwandishi wa makala haya ni miongoni mwa wanachama wake na alisoma ujumbe huo. Membe alieleza kuwa atakwenda ofisini kwa Katibu Mkuu wa CCM iwapo atahakikisha...

Rais Magufuli atema cheche anguko la bei ya korosho Tanzania

Panda shuka za zao la korosho nchini Tanzania zimemvuta Rais John Pombe Magufuli na sasa ametishia tena kuchukua hatua kali. Siku chache zilizopita msimu mpya wa mauzo ya zao la korosho ulifunguliwa huku bei ya zao hilo zikishuka maradufu. Korosho ndio chanzo kikuu cha fedha na tegemeo la kiuchumi kwa wakazi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania. Wakaazi hao kutokana na unyeti wa sekta hiyo waligomea bei mpya kati ya Sh1,900 mpaka Sh2,700 kwa kilo ikiwa ni anguko la kutoka wastani wa Sh4,000 kwa kilo msimu uliopita. Kutokana na hali hiyo, mbunge wa upinzani na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ambaye amekuwa mwiba kwa serikali ya Magufuli amewaambia waandishi kuwa serikali haiwezi kukwepa lawama. "Badala ya Serikali kulichukulia zao la korosho kama la kimkakati imekuwa haisikii, haielewi, na sasa imeharibu kuku anayetaga mayai ya dhahabu katika nchi yetu," amesema. Jana hiyo hiyo Rais Magufuli alifanya kikao na wanunuzi wakuu wa zao hilo na kuwaeleza kuwa serikal...