![]() |
Maziwa ,kilimanjaro |
Nchini Tanzania wengi wao wanaposikia ATM kitu cha kwanza wanachoweza kufikiri huenda ikawa ni chombo cha kutolea fedha.
Jambo
ambalo ni tofauti huko Kaskazini mwa Tanzania katika mkoa wa
Kilimanjaro ipo ATM ya kwanza ya maziwa ambayo imeguka kivutio kwa
wakazi wa mkoa huo.
Unaweza ukajiuliza ATM hiyo inafanyaje kazi?
Nancy Manase ni wenyekiti wa umoja wa wanawake wa maziwa
''Uone
labda tulikuwa tunauza lita mia tatu kwa siku au mia nne sasa
tumeongezea lita mia moja juu kwahiyo ni faida na msimu huu ni ule msimu
unaokuwa na maziwa mengi sana huku kwetu maziwa yanakuwa mengi mpaka
yanamwagwa kwahiyo mpaka sasa hivi hatujamwaga maziwa''.
ATM inatusaidia na watu wamepata elimu kunywa maziwa ni afya kwa sababu hata usipokula kitu kingine inakutosha''
Kila lita moja inagharimu wastani wa dola moja
Lakini katika mashine hii unaweza kununua maziwa ya kiwango chochote kulingana na hela ulionayo
![]() |
Maziwa |
''Kwa muda mfupi niliokuwa hapa katika ATM hii ya
maziwa mkoani Kilimanjaro changamoto kubwa inayo ukabili mradi huu
uliotokea kupendwa na walio wengi ni nishati ya umeme iwapo umeme
utakatika basi ni vigumu kuipata huduma''
Wafugaji mmoja baada ya mwingine huleta maziwa yao hapa kwa ajili ya vipimo na kuandaliwa tayari kwenda kwenye ATM
![]() |
Mashine ya kununulia maziwa |
Kwa upande wa wafugaji wanasema wameanza kuyaona matunda ya uwepo wa ATM hizi
Aleningwasa Swai ni mfugaji ambaye ananufaika na huduma hii.
"Maziwa
yalikuwa hayana bei yalikuwa yananunuliwa kirojorojo tu, lakini tangu
huu mradi ulipoanza wa kupeleka maziwa mjini tumepata faida sana ,
maziwa yanachukuliwa mwisho wa mwezi unakwenda kuchukua hela yako''.
Kwa wateja wa maziwa kwenye ATM nao walikuwa na maoni yao kuhusu mradi huu
"Maziwa
ni mazuri nimeshakunywa maziwa sehemu nyingi, maziwa ya hapa nimeona
kuna utofauti kidogo, cha kwanza maziwa yatoka kwenye ATM halafu istoshe
maziwa ni mazuri kwa hiyo muda wote mtu ukihitaji maziwa ya kuchemsha
na chai unapata muda wowote'', anaeleza mteja wa maziwa, Martin Karata
''Huduma
hii ni nzuri ukija kwa muda wowote unapata maziwa, ikiwa asubuhi mchana
jioni unapata maziwa,"Neema Munisi ni mteja pia.
Kwa sasa zipo ATM mbili tu kwa mkoa mzima
Na walio wengi wanatamani ziongezwe na kusambaa katika maeneo yenye mikusanyiko ya watu
Kama kwenye vituo vya mabasi, Hospitalini na hata sokoni.
Comments
Post a Comment
Here