Beyonce amefichua nyimbo zilizomo
kwenye albamu yake mpya itakayoambatana na filamu mpya The Lion King
remake na albamu hiyo imejumuisha wasanii nyota na wa juu wa muziki
kutoka Afrika.
Wasanii wa Nigeria Tiwa Savage na Mr Eazi
wanatumbuzia katika wimbo wa 'Keys to the Kingdom', wengine Tekno na
Yemi Alade katika kibao 'Don't Jealous Me'.
Burna Boy ana kibao
cha kipekee au solo, 'Ja Ara E', huku msanii wa Cameroon Salatiel
akionekana akiimba na Beyonce na Pharrell Williams katika kibao 'Water'.
Wasanii wengine wa Afrika ni pamoja na Wizkid wa Nigeria, Shatta
Wale wa Ghana, na Busiswa na Moonchild Sanelly kutoka Afrika kusini.
Alipotangaza mpango huo kwa mara aya kwanza wiki iliyopita,
Beyonce alisema "Ilikuwa ni muhimu kuwa muziki usiimbwe na wasanii nyota
na wenye vipaji bali iandaliwe na waandaaji wa Kiafrika. Ubora na moyo
(mapenzi) vilikuwa vitu muhimu kwangu.
"Ni mchanganyiko wa kila kitu, si sauti moja tu. Kuna ushawishi kutoka kila kona, kutoka kwenye R&B, hip-hop na Afro Beat."
Albamu hiyo ka jina 'The Lion King: The Gift', inatarajiwa kuzinduliwa Ijumaa hii.
Inajumuisha
pia vibao vya ushirikiano na wasanii wa Marekani kama Kendrick Lamar,
Pharrell Williams, Childish Gambino, na binti yake Beyonce, Blue Ivy
miongoni mwa wengine.
Ni
kibao tofauti kilichotumika kuisindikiza filamu hiyo ya The Lion King,
Spirit, chenye mistari ya kiswahili, hatahivyo kimejumuishwa pia kwenye
albamu hiyo.
Comments
Post a Comment
Here