Karl Lagerfeld: Mbunifu wa mitindo amrithisha paka wake Choupette sehemu ya utajiri wake wa mamilioni ya dol
Taarifa zimeibuka kwamba mbunifu mavazi aliyeaga dunia Karl Lagerfeld amemuachia paka wake sehemu ya utajiri wake wenye thamani ya $ milioni 200. Mbunifu huyo, raia wa Ujerumani, ambaye alikuwa mbunifu mkurugenzi wa kampuni za Chanel na Fendi, alifariki Paris Jumanne. Alimlea paka wake wa dhati na alivutia ufahari aliokuwa nao kwa paka wake Choupette tangu alipokabidhiwa mnamo 2012. Lagerfeld ameliambia jarida la Ufaransa Numero mwaka jana kwamba amemueka paka huyo kwenye wasia wake kama mmoja wa warithi wa makaazi yake ya kifahari. Katika mahojiano hayo, alisema Choupette yumo ndani ya urathi, 'miongoni mwa wengine'. Lakini ameongeza : "Usijali kuna mali ya kumtosha kila mtu." Haki miliki ya pich GES Image caption Lagerfeld akiwa karibu na mchoro wa Choupette Tayari Choupette ana utajiri wa kiasi, akiwa amejipatia $ milioni 3 kutokana na matangazo ya biashara kwa kampuni ya magari Ujerumani na kampuni ya vipodozi ya Japan akiwa na mmiliki wake Lagerfeld. ...