Shirika la Boeing lilipoamua kuunda ndege yake chapa 747 - lilijizolea sifa kwa kufungua mlango wa kutengeneza ndege kubwa zaidi duniani.
Hata hivyo shirika hilo lililazimika kujenga kiwanda kikubwa zaidi ambacho kina uwezo wa kukidhi mahitaji ya ndege hiyo.
Ikiwa umewahi kuona ndege aina ya 747 ikiwa karibu, bila shaka utafahamu ukubwa wa ndege hiyo.
Kwa hivyo si ajabu kuona kiwanda kilichounda ndege hiyo kuishia kuwa na jumba kubwa zaidi la kiwanda.
Jengo kubwa kiasi gani?
Boeing ilianza kujenga kiwanda cha Everett mwaka 1967, muda mfupi baada ya mradi wake wa Boeing 747 kuanza kushika kasi.
Bill Allen, mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu katika kampuni ya Boeing, anasema shirika hilo lilifahamu fika kuwa, linahitaji sehemu kubwa, endapo lina mpango wa kuunda ndege ya kubeba abiria 400.
Waliamua kuchagua eneo la takriban kilomita 35 Kaskazini mwa jiji la Seattle, karibu na uwanja wa ndege ambao ulitumika kama kituo cha vita wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.
Ripoti katika jarida la Daily Herald liliangazia eneo hilo lililokuwa tu na barabara ndogo mno ya kufikia barabara kuu ya lami, na hakukuwa na njia ya reli kabisa kuunganisha eneo hilo, huku ukizungukwa na msitu ambao ulikuwa makao ya dubu, waliokuwa wakirandaranda humo.
Wakakati huo huo, Boeing ilikuwa ikijenga mojawepo ya uwanja mkubwa zaidi wa ndege duniani, pia kujenga kiwanda kikubwa zaidi cha kuunda ndege, kuwemo uwanjani humo.
Leo, Kiwanda cha Everett kinapiku jumba lolote lile duniani kwa ukubwa na upana, huku kitabu cha kuandika maswala ya maajabu ya dunia- The Guenness Book of Records, kikiripoti kuwa jumba hilo lina ukuwa wa mita za upana milioni13.3 sawa na futi milioni 472.
"Tulijenga jumba hilo kubwa juu ya baadhi ya maeneo maarufu sana duniani," anasema David Reese, ambaye alikuwa akisimamia usafiri wote wa utalii wa kampuni ya Everett. "Tuko na maeneo maarufu kama vile Versailles, Vatican na Disneyland, na unayaona mara tu unapoanza ziara ya kuzuru kiwanda chetu.
Jumba kuu la Everett, linakaa juu ya ekari 97.8 ya ardhi, mara ukubwa mra 30 zaidi ya viwanja maarufu vya Trafalgar Jijini London.
"Nakumbuka nikifanya mahojiano na BBC miaka michache iliyopita, na nikajiuliza, 'hivi uwanja wa Wembley unaukubwa kiasi gani? Naam, jawabu lake ni kuwa uwanja huo unaingia mara 13 ndani ya eneo lote la kiwanda chetu."
Hadi sasa kampuni ya Everett ingali ikiunda ndege chache za aina ya 747, lakini kwa sasa imejiwekeza zaidi kwenye uundwaji wa aina ndogo za 767, 777 na 787. Hata hivyo, ili kutengeneza ndege hizo, angali eneo kubwa hilo linahitajika
Comments
Post a Comment
Here