Skip to main content

Dermophis donaldtrumpi: Kiumbe anayeishi baharini na nchi kavu apewa jina Donald Trump


 Composite image showing the Dermophis donaldtrumpi with photoshopped hair, and US President Donald Trump
EnviroBuild, ndio kampuni iliyopata haki ya kumpa kiumbe huyo jina, iliongeza nywele bandia kwenye kiumbe huyo jambo lililomfanya kuwa na muonekano unaokaribiana na wa Trump.
Kiumbe anayeweza kuishi baharini na katika nchi kavu amepewa jina la Rais wa Marekani Donald Trump, ingawa huenda kiongozi huyo asitake kuhusishwa na kiumbe huyo kutokana na sifa zake.
Amfibia huyo huwa anafukia na kuficha kichwa chake mchangani anapokabiliwa na hatari, jambo ambalo pengine limewashawishi wahusika kumpa kiumbe huyo jina la Trump kutokana na kiongozi huyo kukana kwamba shughuli za viwanda na za kibinadamu zinachangia mabadiliko ya tabia nchi.

Kiumbe huyo pia ni kipofu, hawezi kuona.
Mnyama huyo ambaye amepewa jina Dermophis donaldtrumpi, aligunduliwa katika eneo la Panama, na alipewa jina hilo na mkuu wa kampuni ya EnviroBuild ambaye alikuwa amelipa $25,000 (£19,800) kwenye mnada kupata fursa ya kumpa jina kiumbe huyo.
Kampuni hiyo imesema inataka kuhamasisha watu kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.
"[Dermophis donaldtrumpi] huathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi na kwa hivyo ni kiumbe aliye katika hatari ya moja kwa moja ya kuangamia kutokana na sera ya somo wake kuhusu mazingira," mwanzilishi mwenza wa EnviroBuild, Aidan Bell, amesema kupitia taarifa.
Dermophis donaldtrumpi
Kiumbe huyo mdogo ni wa aina ya caecilian, ambao ni viumbe watelezi wanaofanana na minyoo au nyoka, na huishi sana chini ya ardhi.
Bw Bell amesema tabia za kiumbe huyo zinashabihiana sana na za Trump.
"Kupuuza mambo (sawa na kuficha kichwa mchangani) humsaidia Donald Trump kukwepa maafikiano kuhusu madhara ya mabadiliko ya tabia nchi," amesema.
The Dermophis donaldtrumpi, which was discovered in Panama
Wanasayansi duniani wanakubaliana kwamba mabadiliko ya tabia nchi yanasababishwa na shughuli za kibinadamu.

Lakini Bw Trump, ambaye utawala wake umekuwa ukiendeleza matumizi ya mafuta yanayotokana na kaboni, amewatuhumu wanasayansi hao kwa kuwa na "ajenda ya kisiasa" na kutilia shaka kwamba binadamu wanahusika katika ongezeko la joto duniani.

Comments

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Je unayafahamu maajabu ya Ziwa Ngosi Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayozungukwa na vivutio vingi vya utalii na vingine inawezekana hata havitambuliwi na wenyeji. Ziwa Ngosi yawezekana kuwa ni miongoni mwa vivutio hivyo. Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...