Skip to main content

Posts

Showing posts with the label TAKWIMU

Fahamu ukweli wa dhana tano kuu kuhusu nyoka na maadhimisho ya nyoka duniani

Huku Tarehe 16 mwezi Juni ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya nyoka duniani mnyama huyo hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika. Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani. Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika. Uso kwa uso na nyoka hatari Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya. Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu. Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. Hebu tuwafahamu zaidi. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES ...

WHO: Idadi ya vijana wanaokufa kwa ajali za barabarani inazidi ya wanaokufa kwa virusi vya Ukimwi

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Ajali za barabarani zinatajwa kuwa ndio zinasababisha vifo vingi vya watoto na vijana duniani, kwa mujibu wa shirika la afya duniani(WHO). Shirika hilo la afya limechapisha ripoti ambayo inabainisha kwamba bara la Afrika ndilo lina ajali nyingi za barabarani duniani. Katika taarifa nyingi zinasema kwamba waafrika na wamarekani wa Kusini bado hawana sheria nzuri za kudhibiti mwendo kasi. Lakini taarifa hizo zimesisitiza kwamba vifo vinavyotokana na ajali za barabarani duniani huwa zinalingana na kiwango cha idadi ya watu. Ajali za magari ndio zinaongoza duniani kusababisha vifo kwa watoto na vijana wenye umri kati ya miaka mitano mpaka 29, ripoti hiyo imesema. Ripoti hiyo pia imeeleza kwamba watu wengi zaidi wanakufa kutokana na ajali za barabarani kuliko virusi vya ukimwi , kifua kikuu au magojwa ya kuhara. "Vifo hivyo havikubaliki, hakuna sababu inayoweza kutetea matukio hayo .Hili ni tatizo ambalo linaweza kutafutiwa ufumbuzi" ...