Bw Kabila anasema bado safari ni ndefu Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amesema ataendelea kushiriki katika siasa nchini humo hata baada ya kuondoka madarakani baada ya uchaguzi utakaofanyika wiki mbili zijazo. Aidha, hajafutilia mbali uwezekano wake wa kuwania tena urais uchaguzi mkuu mwingine utakapoandaliwa mwaka 2023. Bw Kabila alitarajiwa kuondoka madarakani miaka miwili iliyopita baada ya kuongoza kwa mihula miwili kwa mujibu wa katiba. Hata hivyo, uchaguzi mkuu nchini humo uliahirishwa mara kadha, serikali ikisema maandalizi yake hayakuwa yamekamilika vyema. Upinzani ulitazama hilo kama njama ya Bw Kabila kutaka kuendelea kuongoza. Mwezi Agosti, Bw Kabila alimtangaza mshirika wake wa karibu Emmanuel Ramazani Shadary ambaye ni waziri wa zamani wa mambo ya ndani kuwa mgombea wa muung...
BLESSED TO BLESS OTHERS