Shirika la ndege la
Fastjet Airlines Limited maarufu kama Fastjet Tanzania limepewa makataa
ya siku 28 kueleza sababu zinazoweza kuzuialisifungiwe kuendelea kuhudu
Tanzania.
Kwa mijibu wa Mamlaka ya Safari za Anga Tanzania,
shirika la ndege la Fastjet limekosa sifa ya leseni ya usafiri wa anga
kwa sababu halina ndege zozote kwa sasa.TCAA imesema ilitoa notice ya siku 28 ya kulitaka shirika hilo lisitishe mauzo kwa abiria. Na limeamuru shirika hilo kurejesha pesa kwa abiria hao au kuwatafutia usafiri katika mashirika mengine.
Mamlaka hiyo pia imeamuru waliopata hasara wafidiwe kwa mujibu wa sheria, na watoe mpango mkakati kwa nini wasifutiwe leseni ndani ya siku 28, pia ikitokea shirika hilo limefungwa basi walipe stahiki za wafanyakazi.
Fastjet tayari wametangaza kusitisha safari zake zote za mwezi Desemba na mwezi Januari. Na wameahidi kurejesha nauli za abiria wote kuanzia tarehe 20 mwezi desemba mwaka 2018.
Katika taarifa yao kwa umma Fastjet wameomba radhi kwa wateja wao bila kuweka wazi utaratibu wa awali kwa hifadhi za wateja hao mpaka watakapo rejeshewa nauli siku chache zijazo.
BBC ilizungumza na mmiliki wa shirika la Fastjet Tanzania Lawrence Masha siku chache zilizopita ambapo aliomba radhi kwa wateja wapya na kufafanua kuwa anafanya awezalo kuingiza ndege nchini.
"Nawaomba radhi sana wateja wangu na malalamiko yao nadhani yataendelea kwa siku moja au mbili. Na nimeingia gharama ya kuingiza ndege nyingine ili kuweza kuwahudumia na nitaingiza ndege ya pili," Bw Masha aliambia BBC.
"Lazima ieleweke kwamba Fastjet PLC ambayo ndio iliyokuwa mmiliki wa Fastjet tanzania wao walikuwa hawana ndege, mimi sijanunua shirika ambalo lilikuwa na ndege nimenunua shirika ambalo lilikuwa na haki ya kutua.
"Kazi yangu ni kuhakikisha naleta ndege ambazo zinaweza kubeba abiria waliopo."
Hata hivyo mmiliki huyo ambaye amenunua asilimia 68 ya hisa za shirika hilo la ndege hivi karibuni ana changamoto kubwa ya kuhakikisha anaingiza ndege hizo alizoahidi kununua kabla Mamlaka ya anga TCAA haijawapokonya kibali.
Katika msimu huu wa sikukuu ambapo idadi ya wasafiri huongezeka, shirika hilo limeacha abiria wake solemba katika mikoa mbali mbali kama vile Dar es salaam na Mwanza huku baadhi ya abiria wakionekana kulalamika katika vyombo vya habari vya ndani na mitandao ya kijamii.
Shirika la Fastjet lilianza kupata mushikeli wa kifedha baada ya mmiliki wa awali Fastjet PLC aliyekuwa na asilimia 49 kujiondoa ambapo shirika hilo liliuzwa kwa wawekezaji wa ndani.
Shirika hilo lilianzishwa mwaka 2011 likifahamika kama Fly540 Tanzania, lakini baada ya kununuliwa kikamilifu na Fly540 mwaka 2012, lilibadilishwa jina na kuwa Fastjet Tanzania.
Comments
Post a Comment
Here