Skip to main content

Jinsi mmea uliopandwa na wanaanga wa China ulivyoota mwezini na kukauka

Hii ni mara ya kwanza mimea inapandwa mweziniHaki miliki ya pichaAFP/CHONGQING UNIVERSITY
Mmea uliopandwa na wanaanga wa China mwezini umechukua takriban siku nane kuota.
Chombo cha angani Cha china kwa jina Change4 kiliwacha kunyunyuzia maji mbegu hiyo ya pamba kama ilivyopangwa nna Chuo kikuu cha Chongqing ambacho kilitunga jaribio hilo.
China ilipata mmea wa kwanza mwezini na kwa nini ni muhimu kuendelea na uchunguzi angani
Mmea huo uliota katika chombo ndani ya Change4 ambacho kilitua katika eneo la mbali la ,mwezini mnamo tarehe 3 Januari.
Eneo ambalo mmea huo ulikulia usingeweza kuishi katika usiku wa mchana wa Lunar Eclipse.
Chombo cha China kilielekea mwezini Change4Haki miliki ya pichaCNSA
Wakati huo wote Ujumbe wote wa China utalazimika kulala na mifumo yao yote italala ili kuhifadhi kawi.
Hivyobasi mmea huo haukunyunyuziwa maji na kulazimika kufa , kama ilivyokuwa imepangwa.

Majaribio mengine

Chombo hicho cha China pia kilibeba mbegu za viazi na arabidopsis, mmea kutoka kwa jamii ya haradali pamoja na matunda na na mayai ya chuchu.
Ilitarajiwa kuwa nyuzi joto duniani zitashuka hadi vipimo vya 52 ili viumbe hao wagande, chuo hicho kilisema katika taarifa siku ya Jumane.
wakati nyuzi joto zinapoanza kupanda mwezi ujao, viumbe vitaruhusiwa kuoza katika chombo kilichozibwa.
Chombo hicho cha Change4 kilizuru baadhi ya maeneo ya mwezi 2013Haki miliki ya pichaCNSA
Baadhi ya matokeo yalishangaza matarajio yetu, alielezea mtunzi wa jaribio hilo , Xie Gengxin, taika runinga ya China.
Uwezo wa kupanda mimea mwezini ni muhimu katika uchunguzi wa siku zijazo angani , ziara kama vile za sayari ya Mars ambayo itachukua takeriban miaka miwili na nusu kuwasili inakoenda.
Hiyo itamaanisha kwamba wanaanga watweza kupanda vyakula vyao angani , wakipunguza haja ya kurudi duniani ili kubeba chakula zaidi.

Je China inatafuta nini katika eneo fiche la mwezini?

Nadhani kuna hamu kubwa katika katiika kuutumia mwezi kama kituo hususana kwa safari za kuelekea sayari ya Mars kwa kuwa ni karibu na duniani, Watson alisema.

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...