Skip to main content

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema oparesheni imekamilika

vikosi vya usalama KenyaHaki miliki ya pichaEPA
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote ''wameangamizwa''.
Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14.
Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano)
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio.
Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo.
ramani
Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo.
Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki katika mkasa huo ni watu 24.
Raia wa Marekani ni miongoni mwa waliyofariki, imesema wizara ya mambo ya nje ya Marekani.
Raia mmoja wa Uingereza pia anahofiwa kufariki dunia.
baadhi ya washambulizi waliyonaswa na camera za CCTVHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWashambuliaji wawili walinaswa na camera za CCTV wakiingia kwenye jengo lililoshambuliwa
"Sasa naweza kuthibitisha kuwa oparesheni ya usalama katika jengo la Dusit imekamilika mna magaidi wote wameangamizwa," alisema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.
"Tutahakikisha kila mmoja aliyehusika na shambulio hili kwa njia moja au nyingine iwe ni kupanga, kufadhili ua kutekeleza shambulio atakabiliwa vikali," ameapa kuwa serikali yake hatachelea kuwakabili vikali''.
"Hili ni taifa linaloongozwa kupitia sheria - taifa ambalo linajivunia amani upendo na umoja ... Lakini ni lazima ieleweke kuwa hatuwezi kuwaachilia huru wale wanaotudhuru sisi na watototo wetu."
Map
Map
Nini kilichotokea?
  • Mashambulizi yalianza saa 9 alasiri saa za Afrika Mashariki.
  • Mashuhuda wanasema waliwaona watu wanne wenye silaha wakiingia kwenye viunga hivyo.
  • Milio mikubwa ya mabomu ilisikika mwanzoni mwa mashambulizi
  • Milio ya risasi bado imeendelea kusikika.
  • Kundi la kigaidi la al-Shabab lenye maskani yake nchini Somalia lilidai kutekeleza shambulio hilo.
  • IGP Joseph Boinnet alithibitisha wahalifu wenye silaha bado wangali ndani ya jengo na vikosi maalumu vya usalama vinapambana nao.
Mwanamke anaefanya kazi katika jengo jirani aliiambia shirika la habari la Reuters kuwa : "Nilisikia milio ya risasi na mara baada ya hapo nikaona watu wakikimbia wkiwa wananyoosha mikono yao juu wengine walikua wakikimbilia kwa benki ili kyanusuru maisha yao."
Vyombo vya habari nchini Kenya vimetoa mkanda wa video kutoka kwenye moja ya kamera za CCTV ikionesha watu waliojihami kwa silaha wakiingia viunga vya hoteli ya DusitD2.
Kamera hizo zimenasa watu wanne wanaoaminika kuwa ni wanamgambo wa al-Shabaab wakiingia kwenye eneo la kuegesha magari ambalo ndio lango kuu la viunga hivyo.
Kuna ripoti kuwa wanne hao waliwahi kuonekana katika eneo la tukiosiku za hivi karibuni.
Saa tano usiku waziri wa usalama, Fred Matiang'i alisema kuwa maafisa wa usalama wamethibiti hali ya usalama katika jumba hilo
"Hali imethibitiwa na nchi ni salama,"aliwaambia wanahabari. "Magaidi hawawezi kutushinda."
Lakini saa kadhaa baadae milio ya risasi iliripotiwa katika eneo la tukio.
Makabiliano makali ya risasi ilisikika mwendo wa saa moja asubuhi saa za Kenya.
Vikosi vya usalama vilifanya msako katika jengo hilo ambapo waliwapata wafanyikazi waliyokuwa wamejawa na uoga wamejificha wengine chini ya viti, meza na hata bafuni
Kufikia alfajiri ya Jumatano mamia ya watu walikua wameokolewa kutoka jumba hilo.
Karibu watu 30 wanaendelea kupokea matibabu katika hospitali kadhaa za Nairobi, vilisema vyombo vya habari nchini humo.
Washambuliaji hao wanasemekana walikimbilia ghorofa ya saba ya jengo hilo ambako watu walikuwa wamejificha.
Eneo la shambulio jiji NairobiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMwathiriwa akisaidiwa kutoka eneo la shambulio
Hoteli ya DusitD2 ina jumla ya vyumba 101 rooms na ipo kilo mita chache nje ya jiji kuu la Nairobi
Kenya imeshuhudia mashambulio kadhaa ya kigaidi katika miaka ya hivi karibuni
Vikosi vya Kenya pia ni sehemu ya vikosi vya kikanda kulinda usalama nchini Somalia.

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...