Hoteli ya DusitD2 Nairobi: Washukiwa watano wa shambulio la Dusit wawasilishwa mahakamani wakificha nyuso zao
Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani .
Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada.
Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea.
Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 .
Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao.
Ni washukiwa wa kwanza kuwasilishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2 . Lakini hawakusomewa mashtaka yao.
Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa.
Washukiwa wanne ni raia wa Kenya huku wa tano akiwa raia wa Canada mwenye mizizi ya Kisomali.,
Mapema maafisa wa polisi waliambia BBC waliwakamata watu saba.
Mtu mmoja ambaye alionekana na washukiwa hao kabla ya shambulio anaaminika kuwa miongoni mwa wale waliozuiliwa lakini hakuwasilishwa mahakamani mapema leo.
Fahamu kuhusu washukiwa waliokamatwa
Watu tisa wametiwa mbaroni kuhusiana na shambulio dhidi ya hoteli ya kifahari mjini Nairobi, Kenya ambapo watu 21 waliuawa.
Washambuliaji wote watano waliyovamia hoteli ya DusitD2 na majengo yaliyokuwa karibu na hapo waliuawa, maafisa walisema huku msako wa kuwatafuta wale waliowasaidia kupanga shambulio hiloukiendelea.
Kundi la al-Shabab lenye makao yake nchini Somalia lemekiri kuhusika na shambulio hili la siku ya Jumanne.
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema kuwa watu wote waliokuwa hawajulikani waliko wamepatikana.
Kumekuwa na taarifa za kukinzana kuhusu mwanamke anayetuhumiwa kuwa mke wa mojawapo ya washukiwa wa shambulio hilo, anayearifiwa alikamatwa Kiambu kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi.
Polisi inasema haiwezi kuthibitisha au kupinga kwamba kuna aliyekamatwa.
'' Hatutaweza kuzungumzia upelelezi wakati huu, kwa mfano tukizungumza kuhusu Kerubo wale waliokuwa karibu na yeye watasikia tumetangaza kuwa tunamtafuta,tunafanya nini...watatoroka'', alisema msemaji wa polisi Charlse Owino.
Aliongeza kuwa cha msingi ni kuhakikisha kuwa wale wote waliyohusika na kupanga na kutekeleza shambulia hilo wanakamatwa.
Tunafahamu nini kuwahusu washambuliaji?
Chombo kimoja cha habari nchini Kenya kinaripoti kuwa anayetuhumiwa kuwa mke wa mmoja wa washukiwa wa shambulio hilo amekamtwa katika eneo la Kiambu, kaskazini mwa mji mkuu wa Nairobi.
Polisi pia inasema kuwa imemtambua Ali Salim Gichunge, anaefahamika kwa jina lingine kama Farouk, kupitia gari lililotumika kufanya shambulio hilo.
Majirani wameliambia gazeti la The Standard kwamba Ali Salim Gichunge na mke wake walihamia mtaa huo mwezi Oktoba mwaka jana.
Wanasema kuwa wawili hao walikua wasiri sana na kwamba walitangaza kuuza vyombo vyao kabla ya shambulio hilo wakisema ''wanahama Nairobi wiki hii".
Al-Shabab walitoa taarifa kuhusiana na shambulio hilo wakisema kuwa ''tunalipiza kisasi uamuzi tata wa rais wa Marekani Donald Trump kutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa Israel''
Msemaji wa baraza la usalama katika ikulu ya White House amejibu taarifa hiyo akisema: "Shambulio hili ni ishara inayotilia mkazo azma ya Marekani ya kukabiliana na ugaidi."
Je wavamizi walitekeleza vipi shambulio hilo?
Shambulio hilo lilianza mwendo wa saa tisa jioni siku ya Jumanne wakati wapiganaji wanne walirusha mabomu katika magari yaliokuwa yameegeshwa kabla ya kuingia ndani ambapo mmoja wao alijilipua, kulingana na maafisa wa polisiSiku ya Jumanne rais Uhuru Kenyatta alisema kuwa wanamgambo wakijihadi waliotekeleza shambulizi hilo ''waliangamizwa'' na vikosi vya usalamabaada ya saa 19.
Kufikia mwendo wa saa tano waziri wa usalama Fred Matiang'i alisema kuwa ,usalama umeimarishwa katika majengo yote yaliokuwa katika eneo hilo.
''Usalama umeimarishwa na taifa lipo salama'' , aliambia wanahabari. ''Ugaidi hautatushinda''.
Lakini saa moja baadaye ufyatulianaji wa risasi na milipuko iliripoitiwa katika eneo hilo.
Kulikuwa na ufyatulianaji mwengine mkali mwendo wa saa moja.
Maafisa wa usalama walilipekua eneo hilo na kuingia ambapo walikutana na wafanyikazi walioogopa. Alafajiri siku ya Jumatano , zaidi ya watu 100 waliokolewa.
Ramani ya Hoteli ya DusitD2 Nairobi
Hoteli hiyo ya DusitD2 ina vyumba 101. ikiwa katika eneo la Westlands , dakika chache kutoka katikakati mwa jiji la Nairobi ina migahawa kadhaa.
Kenya imeshuhudia visa kadhaa vya mashambulizi katika siku za hivi karibuni-hususan katika maeneo yaliopo karibu na Somalia pamoja na mji mkuu wa Kenya.
Kwa jumla watu 700 waliokolewa kutoka jengo hilo, maafisa walisema.
28 kati ya hao wanauguza majeraha katika hospitali tofauti jijini Nairobi.
Baadhi ya wale waliyouawa walikua wakila chakula cha mchana katika mgahawa wa Secret Garden restaurant.
Miili mingine ilipatikana katika ghorofa ya tatu ya jengo la hoteli ya DusitD2.
Can't imagine
ReplyDelete