Skip to main content

Samaki wa Mexico walio na uwezo wa kurekebisha matatizo ya moyo

The Mexican tetra fishHaki miliki ya pichaBHF
Image captionSamaki wa tetra anayeishi katika mito kaskazini mwa Mexico wanaweza kuponya mioyo yao
Samaki anayeweza kuurekebisha moyo wake huenda ndio suluhu ya matibabu kwa watu wenye matatizo ya moyo, kwa mujibu wa utafiti.
Wanasayansi wanao wachunguza samaki wa Tetra kutoka nchini Mexico wamegundua maeneo matatu ya mfumo wa samaki huyo uliochangia uwezo wake kuunda upya tishu za ndani ya moyo.
Jeni moja imeonekana kuwa na jukumu kuu katika mfumo huo.
Watafiti wanatumai utafiti wao siku moja utafanikisha uponyaji wa misuli ya ndani ya moyo kwa wagonjwa ambao wamewahi kupata mshtuko wa moyo.
Maelfu ya watu huishi na matatizo ya moyo baada ya kupata mshtuko wa moyo.
Kwasababu binaadamu hawawezi kuunda upya msuli ulioharibika, au kujeruhiwa kwa moyo, na mara nyingi watu hulazimika kuishi na hali hiyo au kuishia kufanyiwa upandikizaji wa moyo.

Dalili za samaki kwenye pango

Kwa utaifiti huu, uliofadhiliwa na taasisi ya British Heart Foundation, Dkt Mathilda Mommersteeg na kundi lake la wataalamu katika chuo kikuu cha Oxford walichunguza aina mbili za samaki hao aina ya Mexican tetra fish - wanaoishi mitoni, walio na uwezo wa kujiponya, na wengine wanaoishi katika mapango ambao hawana uwezo huo.
Samaki hao wa pangoni ambao kwa wakati mmoja walikuwa wakiishi katika mito kaskazini mwa Mexico walisombwa hadi katika mapango miaka milioni 1.5 nyuma na waligeuka, na kupoteza uwezo wa kuona na rangi ya ngozi kutokana na kuishi kwenye giza.
Kwa kulinganisha aina hizo mbili za samaki, watafiti wamegundua jeni mbili - lrrc10 na caveolin - zilidhihirika zaidi katika samaki wanaoishi katika mito, baada ya kupata majeraha ya moyo.
Samaki wanao kanda miguu katika bwawa la Chemka Tanzania
Baada ya kuligundua hili, waliifungia jeni ya lrrc10 ndani ya viumbe kadhaa vilivyo na uwezo wa kujitibu, kwa zebrafish.
Baada ya kufungwa na kushindwa kufanya kazi vizuri kwa jeni hiyo, samaki huyo wa zebrafish alishindwa kujirekebisha moyo.
Jeraha la tishu linazuia msuli wa moyo kupiga vizuri na kupunguza uwezo wa moyo kusukuma damu mwilini.
Jeni zote mbili zipo ndani ya mwili wa binaadamu.
Dr Mathilda Mommersteeg and a colleague in the Panchon caveHaki miliki ya pichaBHF
Image captionDr Mathilda Mommersteeg and a colleague in the cave where the fish live
Wahariri wa utafiti huo wanasema unadhihirisha siku moja itawezekana kuunda upya sehemu za moyo zilizoharibika ndani ya binaadamu kwa kukarabati namna jeni hizi zinavyofanya kazi.
Hili linawezekana kwa dawa au mbinu za ki elektroniki katika kukarabati jeni ambapo vina saba au DNA inageuzwa, kufutwa au kabdilishwa kwa kutumia vifaa kama Crispr-Cas9.
"Ni hatua za kwanza lakini tuna furaha kubwa kuhusu samaki hawa na uwezekano wa kubadili maisha ya watu wenye matatizo ya moyo" amesema Dkt Mathilda.
Hatahivyo ameongeza kwamba kazi zaidi inahitajika kutafuta jeni nyingine muhimu ambazo huenda zikatumika katika kusahihisha matatizo ya moyo.
Utafiti huu umechapishwa katika jarida la Cell Reports.

Comments

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...

Je unayafahamu maajabu ya Ziwa Ngosi Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayozungukwa na vivutio vingi vya utalii na vingine inawezekana hata havitambuliwi na wenyeji. Ziwa Ngosi yawezekana kuwa ni miongoni mwa vivutio hivyo. Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.