Skip to main content

Karl Lagerfeld: Mbunifu wa mitindo amrithisha paka wake Choupette sehemu ya utajiri wake wa mamilioni ya dol

ChoupetteTaarifa zimeibuka kwamba mbunifu mavazi aliyeaga dunia Karl Lagerfeld amemuachia paka wake sehemu ya utajiri wake wenye thamani ya $ milioni 200.
Mbunifu huyo, raia wa Ujerumani, ambaye alikuwa mbunifu mkurugenzi wa kampuni za Chanel na Fendi, alifariki Paris Jumanne.
Alimlea paka wake wa dhati na alivutia ufahari aliokuwa nao kwa paka wake Choupette tangu alipokabidhiwa mnamo 2012.
Lagerfeld ameliambia jarida la Ufaransa Numero mwaka jana kwamba amemueka paka huyo kwenye wasia wake kama mmoja wa warithi wa makaazi yake ya kifahari.
Katika mahojiano hayo, alisema Choupette yumo ndani ya urathi, 'miongoni mwa wengine'. Lakini ameongeza : "Usijali kuna mali ya kumtosha kila mtu."
Karl LagerfeldHaki miliki ya pichGES
Image captionLagerfeld akiwa karibu na mchoro wa Choupette
Tayari Choupette ana utajiri wa kiasi, akiwa amejipatia $ milioni 3 kutokana na matangazo ya biashara kwa kampuni ya magari Ujerumani na kampuni ya vipodozi ya Japan akiwa na mmiliki wake Lagerfeld.
Katika mahojiano tofuati na Numero, Lagerfeld amefichua kwamba amemuajiria paka huyo mayaya wawili, ili kumshughulikia, ambaye amesema anakula "vyakula vinne tofuati'' kwa siku anavyotayarishiwa katika 'mabakuli ya aina yake'.
Alimuezesha Choupette kuwa nyota katika mitandao ya kijamii, akiwa na ukurasa wake katika Twitter na Instagram ambazo zina takriban wafuasi 200,000 kwa pamoja.
Presentational white space

Wanyama wanaofugwa kwa fahari na starehe kubwa

Lagerfeld sio tajiri pekee anayetaka kumuachia mnyama anayemfuga mali kushughulikia maslahi yake.
Mbunifu mwingine wa mavazi Alexander McQueen aliacha £50,000 katika urathi wenye thamani ya £16m ili mbwa wake watendekezwe maishani mwao yote.
Bubbles the chimpanzeeHaki miliki ya pichaAGES
Image captionSokwe wa Michael Jackson Bubbles alikuwa akivalishwa nguo sare na mmiliki wake
Lakini sokwe kwa jina Bubbles, aliyemilikiwa kwa wakati mmoja na marehemu muimbaji Michael Jackson, hakuwa na bahati sana.
Alipokuwa mkubwa, na kuanza kuonyesha dalili za ukali, aliepelekwa katika hifadhi ya wanyama pori .
Punde baada ya kuhamishwa, Jackson hakulipa tena malipo ya kushughulikia kwake Bubbles.
Wasimamizi wa makaazi ya muimbaji huyo sasa wanatuma kiasi cha pesa katika hifadhihiyo huko Florida kila mwaka, lakini inaarifiwa sio fedha kamili za kumshughulikia sokwe huyo.
Bubbles amelazimika kujikimu atahivyo. Sehemu ya talanta aliye nayo katika sanaa huuzwa kupata pesa za kukimu mahitaji katika hifadhi hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...