Skip to main content

Boeing 737 Max: Rwanda yapiga marufuku hizo kuruka katika anga yake

Boeing 737 Max 8Haki miliki ya pichaSTEPHEN BRASHEAR
Shirika la usafiri wa ndege Rwanda limetoa agizo kwa marubani na kampuni za ndege kutoendesha ndege za Boeing 737 Max 8 ana 9 katika anga ya Rwanda.
Rwanda sasa imejiunga na mataifa mengine duniani ambayo yamepiga marufuku usafiri wa ndege hizo za aina ya Boeing 787 Max 8 na Max 9.
Hii inafuata ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Jumapili ilioanguaka muda mfupi baada ya kupaa kutoka mji mkuu Addis Ababa na kusababisha vifo vya watu 157
Taarifa zinaeleza kwamba Rwanda ilikuwa na mipango ya kukodisha ndege mbili za aina hiyo Boeing 737- 800.
Hatahivyo, huenda mipango hiyo ikasitishwa kwa muda sasa wakati kukisubiriwa uchunguzi wa chanzo cha ajali ya ndege ya Ethiopia iliyoanguka Jumapili nje kidogo ya mji mkuu Addis Ababa.
Ndege kama hiyo ya kampuni ya Lion Air, ilianguka kutoka pwani ya Indonesia Oktoba mwaka jana na kusababisha vifo vya watu 189.
Katika taarifa rasmi iliyowekwa kwenye mtandao wa twitter ya mkurugenzi mkuu katika shirika hilo la usafiri wa ndege Rwanda, Silas Udahemuka, RCAA limesema kwamba marufuku hiyo imeanza kufanya kazi mara moja.
"Shirika la usafiri wa ndege Rwanda kwa uwezo uliopewa katika kifungu cha 16 cha sheria za usafiri wa ndege nchini inaagiza marubani na kampuni za ndege zinazohudumu ndege za Boeing 737 - 8 Max na Boeing 737 - 9 Max, zisiendeshe usafiri wowote wa ndege hizo katika anga ya Rwanda mara moja," inasema taarifa hiyo.
Marekani ni nchi ya hivi karibuni kusitisha usafiri wa ndege hiyo ya Boeing 737 Max yakiwemo mataifa mengine kama Uingereza, Umoja wa Ulaya, China India na Australia ambayo yote yameamua kusitisha usafiri wa ndege hizo.
Ndege aina ya Boeing 737 Max-8 iliyoanguka JumapiliHaki miliki ya pichaJONATHAN DRUION
Boeing 737 Max yasitisha matumizi ya ndege aina hiyo 'hadiangalau Mei'
Ndege zote za Boeing 737 Max 8 na 9 zimepigwa marufuku kuhudumu hadi angalau Mei baada ya ajali hiyo ya shirika la ndege la Ethiopia, Shirika la kitaifa la usafiri wa ndege nchini Marekani (FAA) limesema.
Ndege hizo hazitohudumu hadi mfumo wake wa uhudumu uimarishwe na uidhinishwe, FAA limesema.
Mkasa huo wa ndege nje kidogo ya mji mkuu Addis ulisababisha vifo vya watu 157 kutoka mataifa 35.
Ni ajali ya pili ya aina hiyo ya ndege ya 737 Max katika muda wa miezi mitano.
Baadhi ya watu wamegusia ufanano wa mikasa hiyo, huku baadhi ya wataalamu wakitaja data ya satelaiti na ushahidi kutoka eneo la mkasa kuonyesha uhusiano wa ajali ya ndege ya Ethiopia na ile ya iliyotokea Indonesia ya Lion Air mwaka jana.
Maafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwa
Wachunguzi nchini Ufaransa wamepokea jukumu la kisanduku kinachonakili data ya safari hiyo ya ndege maarufu 'black boxes' wakijaribu kubaini chanzo cha ajali ya ndege hiyo ya Boeing 737 Max.
Huenda ikachukua muda kupata data ya awali, lakini mengi itategemea hali ya kisanduku hicho.

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...