Waziri wa fedha Tanzania' ametangaza kodi ya 25% kwa uingizaji wa nywele zote bandia maarufu mawigi na 10% kwa zinazotengenezwa nchini katika jitihada za kukuza uchumi wa nchi.
Waziri Philip Mpango ametangaza hatua hizo, ambazo zitaidhinishwa mwanzoni mwa mwezi ujao kama sehemu ya bajeti iliyosomwa jana, ya mwaka 2019 na 2020.Kadhalika kodi kwa visodo imerudishwa kutokana na kwamba hatua ya kuondoshwa kodi mwaka jana kwa bidhaa hizo muhimu kwa wanawake, haikusaidia kushuka kwa bei.
Na badala yake Mpango ameeleza kuwa ni wafanya biashara wanaofaidi kutokana na kuondolewa kwa kodi hiyo.
wanawake wengi huvaa nywele hizo bandia ambazo kwa wingi husafirishwa kutoka mataifa ya nje.
Kwa makadirio, wigi hugharimu kati ya $4 na hata zaidi ya $130.
Hii ina maana kwamba sekta ya urembo ambayo ni muhimu hususan kwa vijana na wanawake, itaathirika katika siku zijazo.
Kodi mya pia inatarajiwa kuidhinishwa Uganda katika siku zijazo kwa vipodozi vinavyoingizwa nchini kukitarajiwa kukusanywa mapato ya hadi shilingi bilioni 11.6 za Uganda ,kutokana na kodi itakayotozwa kwa bidhaa hizo.
Imepokewaje hatua hii?
Wanawake wengi katika makundi ya WhatsApp na mitandao ya kijamii na hata wanaume wamekuwa wakizungumzia kuhusu pendekezo hilo:Baadhi hata wakidhihaki namna wanawake waliozoea kutumia bidhaa hizo, sasa watataabika.
Wengine wakitathmini athari kwa wafanyabiashara na wajasiriamali wanaojishughulisha na uingizaji na utengenezaji wa nywele bandi.
Annasatasia Sigera, mmiliki wa 'Wigs by Vianna' nchini Tanzania anasema ameshtushwa kusikia kutangazwa kwa kodi hiyo.
''Inaweza ikaathiri biashara, kwenye ongezeko la bei na hasaa kwa wauzaji wa ndani ya nchi ambao baadhi wana matawi yao nchini, wanaingiza kutoka China na kuzileta katika maghala yao'..
Anasema anaona kwamba huenda kukawa na shida mwanzoni, lakini mwisho wa kwisha anasema ni kwamba watu wanapenda nywele na watazidi kununua.
Tofauti anaeleza ni kati ya watengenezaji na wanaonunua na kuingiza.
''Sisi ambao tunatengeneza tunajua namna gani ya kubana na kuifanya bei isipande sana, lakini kuna wanaonunua na kuuza kama zilivyo, hao ndio itakayowaathiri zaidi''.
Kadhalika Ana, anasema huenda pia ikaathiri ubora wa nywele zinazoingizwa au kutengenezwa nchini.
Kauli anayokubaliana nayo mpambaji maarufu wa nywele Tanzania, Aristotee aliyetoa wito kwa serikali kutathmini pendekezo hilo.
''Serikali ijaribu kuliangalia hili suala, ni bei kubwa sana.
''Yaani itafanya mpaka hivi vitu viwe bei kubwa zaidi. Ushuru ukipanda maana yake ni kuwa nywele itauzwa bei kubwa zaidi, Mtanzania wa kawaida ataweza kununua wapi?'' anauliza Aristotee.
Kwa upande mwingine Bi Sigera anaeleza kwamba anaitazama hatua hii ya kuidhinishwa kodi kama fursa nzuri inayojitokeza katika kitengo au biashara ya nywele.
Kwamba nywele zinamulikwa, Ana anasema utambulisho huo huenda unaashiria nafasi iliopo kwa wajasiriamali nchini.
''Lakini pia huenda ni fursa ya kuimarisha bidhaa zinazoingizwa nchini'' anasema Annasatsia.
Kodi nyingine zilizopendekezwa Tanzania ni 35% kwa chokleti na biskuti ambazo awali zilikuwa zinatozwa 25%.
Comments
Post a Comment
Here