When preparing raw food, surfaces have to be cleaned thoroughly afterwards. |
Kuosha mikono, nguo na kusafisha sehemu kwa wakati muafaka ndio chanzo cha afya nzuri- lakini mtu mmoja kati ya wanne wanadhani hilo sio muhimu, ripoti hiyo inaonya.
Kulifanya hilo kwa njia sawa kunaweza kupunguza maambukizi na magonjwa kukaidi dawa za antibiotic.
Kuna mchanganyiko kwa umma kuhusu utofuati katiya uchafu na viini vya uchafu au germs, usafina afya.
Katika utafiti wa watu 2,000, asilimia 23 walidhani watoto wanihatji kushika uchafu ili kujenga mfumo wa kinga mwilini.
Lakini wataalamu katika ripotihiyo wanasema "kuna uwezekano wa madhara" yanayoweza kuwafanya kupata maambukizi hatari.
Badala yake, walisema watu wanastahili kuangalia usafi wa maeneo maalum kwa wakati maalum, hata kama maeneo hayo yanaonekana kuwa masafi, ili kuweza kuzuia kusambaa kwa viini vya uchafu.
Ni maeneo gani muhimu yanastahili kusafishwa?
- Maeneo yakupika na kutayarisha chakula
- Kula kwa vidole
- Baada ya kutoka msalani
- Unapokohoa, kupiga chafya au kupangusa kamasi
- Unaposhika au kuosha nguo chafu
- unapowashughulikia wanyama
- unapokusanya au kuondosha taka taka
- unapomhudumia jamaa aliye na kidonda mwili
Kusafisha jikoni na vyombo vya kukatia mboga ni muhimu baada ya kutayarisha vya vyakula vibichi kama mboga na nyama, au kabla ya kutayarisha chakula.
Vitambaa vya jikoni na brashi zinazotumika kwa usafi ni muhimu kuzisafisha baada ya matumizi.
Je usafi unaondosha vipi bakteria?
Kuoshasehemu tunzotumia jikoni kama vibaraza na vyombo kwa maji ya vuguvugu au sabuni husaidia kuondosha bakteria na kuruhusu zishuke kwenye mtari w amaji.
Utumie nini kusafisha?
Ni katik amakundi matatu:
- Sabuni - husafisha na kutoa mafuta lakini haziui bakteria.
- Dawa za kuuwa vidudu - huua bakteria lakini hazisafishi vilivyo maeneo yalio na mafuta na uchafu.
- Dawa za kusafisha - Zinaweza kutumika kusafisha na kuua bakteria.
Badala ya kutumia kitambaa kusafisha maeneo baada ya kupika chakula, tumia karatasi. hii husaidia kuepusha vitambaa vinavyotumika mara kwa mara kubeba uchafu.
Wataalamu wanasemaje?
Profesa Sally Bloomfield, kutoka chuo cha London School of Hygiene and Tropical Medicine, anasema watu wanapaswa kujua tofuati ya afya na usafi.
"Usafi ni kutoa uchafu na vimelea, afya ni kusafisha maeneo na kwa wakati muafaka - kwa namna sahihi kuzuia maambukizi wakati wa kutayarisha chakula, unaptoka msalani au unapowashughulikia wanyama nyumbani."
Profesa Lisa Ackerley, fmtaalamu wa usafiwa chakula na afya anasema: "Kutoka nje na kucheza na marafiki na familia au wanyama ni fursa kwa bakteria kusambaa lakini ni muhimu pia kwa watu kutojipata katika matatizo.
Ameongeza: "Afya nzuri na usafi wa nyumbani na maisha ya kila siku husaidia kupunguza maambukizi, na ni muhimu katika kuwalinda watoto wetu na kuepuka kwenda hospitali mara kwa mara ,na husaidia pakubwa katika kupambana na antibiotiki kukaidi makali ya magonjwa."
Tunashukuru kwa elimu
ReplyDeletepamoja kiongoz
Delete