Skip to main content

Je unayafahamu maeneo muhimu ya kuyasafisha nyumbani kwako?

Cutting up chicken with a knife
When preparing raw food, surfaces have to be cleaned thoroughly afterwards.


       
Watu wanapaswa kufahamu namna ya kuzuia viini vinvayosababisha magonjwa vinavyosambaa nyumbani kliko kufanya usafi wa maeneo wanayoyaona kuwa ni "machafu", kwa mujibu wa ripoti ya British Royal Society for Public Health (RSPH).
Kuosha mikono, nguo na kusafisha sehemu kwa wakati muafaka ndio chanzo cha afya nzuri- lakini mtu mmoja kati ya wanne wanadhani hilo sio muhimu, ripoti hiyo inaonya.
Kulifanya hilo kwa njia sawa kunaweza kupunguza maambukizi na magonjwa kukaidi dawa za antibiotic.

Na hakuna usafi 'unaopita kiasi'.
Kuna mchanganyiko kwa umma kuhusu utofuati katiya uchafu na viini vya uchafu au germs, usafina afya.
Katika utafiti wa watu 2,000, asilimia 23 walidhani watoto wanihatji kushika uchafu ili kujenga mfumo wa kinga mwilini.
Lakini wataalamu katika ripotihiyo wanasema "kuna uwezekano wa madhara" yanayoweza kuwafanya kupata maambukizi hatari.
Badala yake, walisema watu wanastahili kuangalia usafi wa maeneo maalum kwa wakati maalum, hata kama maeneo hayo yanaonekana kuwa masafi, ili kuweza kuzuia kusambaa kwa viini vya uchafu.

Ni maeneo gani muhimu yanastahili kusafishwa?

  • Maeneo yakupika na kutayarisha chakula
  • Kula kwa vidole
  • Baada ya kutoka msalani
  • Unapokohoa, kupiga chafya au kupangusa kamasi
  • Unaposhika au kuosha nguo chafu
  • unapowashughulikia wanyama
  • unapokusanya au kuondosha taka taka
  • unapomhudumia jamaa aliye na kidonda mwili
Dog licking someone's hand                          
Ni muhimu sana kusafisha mikono baada ya kushughulikia chakula, unapotoka msalani unapokohoa au unapowashughulikia wanyama nyumbani, ripoti hiyo imesema.
Kusafisha jikoni na vyombo vya kukatia mboga ni muhimu baada ya kutayarisha vya vyakula vibichi kama mboga na nyama, au kabla ya kutayarisha chakula.
Vitambaa vya jikoni na brashi zinazotumika kwa usafi ni muhimu kuzisafisha baada ya matumizi.
Je usafi unaondosha vipi bakteria?
Kuoshasehemu tunzotumia jikoni kama vibaraza na vyombo kwa maji ya vuguvugu au sabuni husaidia kuondosha bakteria na kuruhusu zishuke kwenye mtari w amaji.

lakini ili kuua bakteria kikamilifu, maji ya moto sana yanahitajika na yamiminwe kwa muda fulani. Shirika la the Food Standards linasema.
Utumie nini kusafisha?
Ni katik amakundi matatu:
  • Sabuni - husafisha na kutoa mafuta lakini haziui bakteria.
  • Dawa za kuuwa vidudu - huua bakteria lakini hazisafishi vilivyo maeneo yalio na mafuta na uchafu.
  • Dawa za kusafisha - Zinaweza kutumika kusafisha na kuua bakteria.
Ni muhimu kusoma maagizo vizuri wataalamu wanasema.
Badala ya kutumia kitambaa kusafisha maeneo baada ya kupika chakula, tumia karatasi. hii husaidia kuepusha vitambaa vinavyotumika mara kwa mara kubeba uchafu.Washing hands after using the toilet                           
Wataalamu wanasemaje?
Profesa Sally Bloomfield, kutoka chuo cha London School of Hygiene and Tropical Medicine, anasema watu wanapaswa kujua tofuati ya afya na usafi.
"Usafi ni kutoa uchafu na vimelea, afya ni kusafisha maeneo na kwa wakati muafaka - kwa namna sahihi kuzuia maambukizi wakati wa kutayarisha chakula, unaptoka msalani au unapowashughulikia wanyama nyumbani."
Profesa Lisa Ackerley, fmtaalamu wa usafiwa chakula na afya anasema: "Kutoka nje na kucheza na marafiki na familia au wanyama ni fursa kwa bakteria kusambaa lakini ni muhimu pia kwa watu kutojipata katika matatizo.
Ameongeza: "Afya nzuri na usafi wa nyumbani na maisha ya kila siku husaidia kupunguza maambukizi, na ni muhimu katika kuwalinda watoto wetu na kuepuka kwenda hospitali mara kwa mara ,na husaidia pakubwa katika kupambana na antibiotiki kukaidi makali ya magonjwa."

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.