Skip to main content

Magufuli amtaka waziri 'avute bangi'

Rais Maguli
Image captionRais wa Tanzania, Dokta John Magufuli ameonyesha kutoridhishwa na utekelezwaji wa miradi ya maji
Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli amemtaka waziri wa maji na umwagiliaji Profesa Makame Mbarawa kuwa mkali kusimamia miradi ambayo imekusudiwa na serikali.
Alipokua kwenye ziara ya kikazi mkoani Njombe, nyanda za juu kusini mwa Tanzania Rais Magufuli amekagua miradi mbali mbali ikiwemo kufungua barabara ya Mafinga mpaka Igawa yenye umbali wa kilometa 138.7.
Kando na hilo Magufuli ameonyesha kutoridhishwa na utekelezwaji wa baadhi ya miradi ya maji nchini Tanzania. Magufuli kwa lugha ya utani alimtaka waziri wa Maji Prof Mbarawa kuvuta bangi ili kuwa mkali.
Amesema katika uhakiki wa miradi ya maji kuanzia mwaka 2013 mpaka 2018 palikua na miradi ya maji iliyohakikiwa na wataalamu kutoka wizara ya fedha ambapo kulikua na miradi ya thamani bilioni 119 miradi ya kweli ilikua na thamani ya bilioni 17.

Kati ya bilioni 119 madai ya kweli ya mradi uliofanyika ni bilioni 17 kwa hiyo miradi mingine yote ilikua hewa.Watu walidai fedha kuwa wamefanya kazi ya miradi ya maji lakini maji hayakuwepo hivyo ni sawa na kusema miradi hewa na hizo fedha hazikulipwa.
Amemueleza waziri wa maji: ''Nimekupeleka pale ukafanye mabadiliko Ili miradi ya maji iliyopangwa hapa makambako yenye thamani ya bilioni 45 na umesema makandarasi watakua kwenye site ikifika mwezi wa tisa, ukalisimamie hilo
Rais Magufuli ameeleza kuwa na matatizo na baadhi ya miradi ya maji nchini hali inayofanya kufanya mabadiliko kwenye miradi ya maji hata kwa mawaziri kwa kuwa haoni faida yake kwa wananchi.
''Zinazungumzwa fedha zimeenda kwenye miradi lakini hazikwenda, kuna wakati nilienda kanda ya ziwa ninauliza mradi wa maji uko wapi zimetumika milioni 400 zilikua milioni 800 lakini maji hayapo''
''Sasa nikuombe waziri na watendaji wako mkawe wakali kweli kweli kama una uwezo wa kuvuta bangi ya njombe ili uwe mkali kaivute, kaivute kisirisiri ili wasikuone ukiivuta ili ukienda kwenye mradi hawa mainjinia wa maji wakafanye kazi''.Alisema Rais Magufuli

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...