
Idara ya hali ya anga nchini Kenya inasema kuwa kiangazi kitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu huku upepo wa mvua ukisalia nchini Tanzania kutokana na kiwango cha chini cha upepo.
Mvua ndefu itaanza kunyesha katika maeneo mengi ya Kenya ifikiapo miwsho wa mwezi huu, wataalam wa hali ya anga wamesema.
Kaimu mkurugenzi wa shirika la hali ya anga nchini Kenya Stella Aura alielezea kwamba upepo wenye mvua umekwama nchini Tanzania kutokana na shinikizo ya kiwango cha chini ambayo haiwezi kuisukuma mvua hiyo kuelekea kaskazini mwa Kenya.
Mwezi Aprili ndio mwezi wa mvua ndefu nchini Kenya na onyo limetolewa katika maeneo kadhaa ya Kenya kuhusu kuchelewa kwake.
''Mvua ya msimu husababishwa na upepo wa mvua unaoelekea kaskazini lakini kufikia sasa upepeo huo haujaelekea kaskazini'', aliambia vyomb vya habari.
''Mvua imekwama nchini Tanzania, mifumo ya upepo iliopo kusini haijashikamana kuweza kusukuma mawingu hivyobasi mvua itachelewa , lakini mvua itaanza kunyesha mwisho wa mwezi huu'', alisema.
Mvua Ndefu
Hatahivyo amesema kuwa mvua ndefu imeanza lakini kwa kiwango kidogo katika maeneo mbalimbali.
Mvua ndefu hunyesha miezi ya Machi, Aprili, na Mei hususan katika eneo la magharibi , bonde la Ufa na mkoa wa kati na ni muhimu sana katika sekta ya kilimo hatua inayosababisha kuwepo kwa chakula cha kutosha.
Idara hiyo imewashauri wakulima kupanda mimea inayokuwa kwa haraka na ile isiotegemea maji kwa kuwa mvua hiyo huenda isinyeshe kwa muda mrefu.
Mafuriko
Wale wanaoishi katika maeneo ya nyanja za chini ikiwemo miji midogo isio na mitaro ya kusafirisha maji walionywa kwamba watarajie mafuriko.
Magharibi mwa Kenya, visa vya radi vinatarajiwa kuongezeka huku maporomoko yakitarajiwa kufanyika katika maeneo ya juu ikiwemo Murang'a na Meru miongoni mwa mengine.
Maporomoko pia yanatarajiwa kuathiri maeneo ya magharibi na mkoa wa Bonde la Ufa.
''Mikakati inafaa kuwekwa ili kuzuia maafo yoyote'' ,ilishauri idara hiyo.
Comments
Post a Comment
Here