
Kipindi cha Televisheni kinachoonesha maihsa ya uhalisi 'Keeping up with the Kardashians' kimeanza upya kwa msimu wa 16, kumaanisha mvutano na malumbano ya familia hiyo yanaywekwa parwanja kwa mara nyingine.
Kipindi hicho kimekuwa kikipeperushwa kwa muda unaozidi muongo mmoja sasa, huku utajiri wa familia huo ukikuwa kwa kadri ya miaka ya kipindi hicho.
Kylie Jenner - ambaye wakati kipindi hicho ha TV kilipoanza alikuwa na miaka 9 - sasa ana miaka 21 na ni bilionea.
Akiwa na utajiri unaokadiriwa $1bn (£760m), kwa mujibu wa jarida la Forbes, mwanadada huyo mmiliki wa kampuni ya vipodozi ndiye aliye tajiri zaidi kati ya wanfamailia nzima ya Kardashian clan, inayoongozwa na kusimamiwa na mama Kris Jenner.
Hatahivyo, ndugu zake wengine pia sio kwamba hawajiwezi.
Kim Kardashian West ni tajiri mwenye mamilioni ya dola kutokana na kampuni yake pia ya vipodozi na manukato; Kendall Jenner ni mwanamitindo wa kimataifa; Khloe Kardashian ana kampuni ya kuuza suruali aina ya jeans na dada mkubwa kabisa Kourtney Kardashian amefaidika kutokana na kushirikishwa katika matangazo ya biashara na kampuni za kutengeneza nguo.
Kwa kuchanganya kazi na maisha binfasi na utajiri unaotokana na uwepo wao katika mitandao ya kijamii umedhihirika kuwnaa faida kubwa kwao.

Alexander McKelvie, mhadhiri kuhusu masuala ya ujasiriamali kutoka chuo kikuu cha Syracuse anamaini pia kipindi chao kimeandikwa vizuri sana.
"Unapokikagua kipindi hicho unaweza kufikiria ni matukio ya papo kwa hapo," amesema.
"lakini huenda tamthilia imeandikwa na kupangwa vizuri kwa ujumbe wa kuvutia kuhusu wasimamizi wa kipindi na familia yenyewe wanachotaka kijulikane kuwahusu."
Familia ya Kardashian imetoa wapi mamilioni ya dola?
Msimu mpya wa kipindi cha Keeping up with the Kardashians kinalenga kuangazia "kashfa" inayowahusu Khloe Kardashian, aliyekuwa mpenzi wake Tristan Thompson na anayeonekana kuwa 'mchepuko' rafiki wa dhati wa Kylie Jenner, Jordyn Woods.
Katika kipindi hicho, Khloe analalamika: "Inaudhi kwamba limekuwa jambolinalojulikana na umma. Sio kwamba ni makala ya Televisheni, haya ni maisha yangu binafsi."
Kwa wakati ambapo kashfa hii ilipofichuka, bei ya rangi ya mdomo 'Jordy Lip Kit', bidhaa iliyotokana na ushirikiano wa Kylie na Jordyn, ilishushwa bei kwa 50%.
Iliuzika mpaka ikamalizika
Ni wazi kwamba kashfa hiyo iligueza hesabu.

Wakati Kylie alipozindua rangi za mdomo mnamo Novemba 2015, alifanikiwa kuwauzia mamilioni ya mashabiki moja kwa moja kupitia mtandao wa kijamii iliomaanisha kwamba alifanikiwa kukwepa gharama ya kunadi bidhaa katika soko na alipata faida ya kujua hisia za watumiaji moja kwa moja iwapo wameipenda au hawakuipenda bidhaa hiyo.
Je familia hii inatengeneza pesa daima?
Baadhi ya mikataba ambayo familia hiyo imefikia katika miaka ya kwanza ya ufahari wao hususan kwa kuwahusisha ndugu zake wakubwa Kourtney, Kim na Khloe, haijakuwa rahisi au shwari.
Dada hao walikuwa sura ya kampen iya vipodozi iliyopewa jina Khroma Beauty kupiitia kibali cha makubaliano.
Lakini baada ya uzinduzi mnamo 2012, vipodozi hivyo viliondolea kutoka madukani kutokana na tuhuma za ukiukaji wa haki miliki.
Baadaye zikarudishwa kwa jina jipya la Kardashian Beauty, lakini bado waliandamwa kisheria. Ni hivi karibuni tu ambapo familia hiyo imefanikiwa kujitoa katika kesi hiyo.

Walizindua pia Kardashian Kard, kadi ya kuchukua bidhaa kwa akiba zilizolengwa vijana na wazazi wanaotaka kufuatilia matumizi ya watoto wao.
Iliondoshwa hatahivyo baada ya aliyekuwa mkuu wa sheria wa jimbo la Connecticut Richard Blumenthal kusema kwamba ana wasiwasi na gharama kubwa ya kadi hizo.
Na hata sasa, sio kila kitu wanachoianzisha kinafanikiwa.
Tangazo la Kendall Jenner na kampuni ya kinywaji Pepsi lilikabiliwa na shutuma kali na hasira dhidi ya tangazo hilo ambalo baadhi waliliona kupuuzia uzito wa mauaji ya watu weusi Marekani kupitia vuguvugu la Black Lives Matter movement.
Pepsi iliondoa tangazo hilo siku moja baada ya kupeperushwa.
Na si hayo tu, familia hiyo imeshutumiwa pakubwa kwa kupokea fedha katika kuendekeza na kuhimiza matumizi ya bidhaa za kupunguza uzito wa mwili.
Comments
Post a Comment
Here