Skip to main content

VYAKULA 10 VINAVYOFAA KWA WANAUME.

See the source image

1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito.
2. Samaki kutoka baharini, asa wenye magamba ambao huwa na virutubisho vya zinc vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu za kiume. Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kuku huwa na kiasi kikubwa cha madini haya.


3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia kuondoa mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya moyo.
4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia.
5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo husaidia kujenga  misuli imara. Pia ina bacteria rafiki wanaosaidia kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo.
6. Ndizi mbivu, Ina virutubisho vya potassium ambavyo uimarisha misuli, mifupa na kupunguza shinikizo la damu.
7. Nafaka, vyakula hivi huongeza nguvu na huwa na nyuzinyuzi kusaidia kupata choo vizuri na kuimarisha mwili wako.
8. Tomato Souce ina virutubisho vya leukopene ambavyo ukulinda dhidi ya saratani ya tezi ya kiume.
9. Mboga za majani na matunda, kama pilipili, machungwa,  karoti, spinachi na maboga zina kemikali na virutubisho vinavyosaidia kuongeza kinga ya mwili, kuzuia kuzeeka mapema na kukukinga na saratani.
10. Mayai, yana virutubisho vya lutein, protini namadini ya chuma yanyosaidia ukuaji wa chembe nyekundu za damu.

Comments

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...

Je unayafahamu maajabu ya Ziwa Ngosi Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayozungukwa na vivutio vingi vya utalii na vingine inawezekana hata havitambuliwi na wenyeji. Ziwa Ngosi yawezekana kuwa ni miongoni mwa vivutio hivyo. Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.