Papa Francis ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumchapa kibao, mmoja wa waumini kwenye kanisa la St Peter's Square huko Rome.
Papa alikuwa akisalimiana na watoto na
mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa
watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu
amuangushe.
Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira.
Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine.
Kitendo
cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala
kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi wakimuunga mkono Papa.
Awali wakati wa hotuba yake ya mwaka mpya, Papa alikemea unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Comments
Post a Comment
Here