Skip to main content

Rais Magufuli atema cheche anguko la bei ya korosho Tanzania

Rais Magufuli na Wairi Mkuu Kassim MajaliwaPanda shuka za zao la korosho nchini Tanzania zimemvuta Rais John Pombe Magufuli na sasa ametishia tena kuchukua hatua kali.
Siku chache zilizopita msimu mpya wa mauzo ya zao la korosho ulifunguliwa huku bei ya zao hilo zikishuka maradufu.
Korosho ndio chanzo kikuu cha fedha na tegemeo la kiuchumi kwa wakazi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania.
Wakaazi hao kutokana na unyeti wa sekta hiyo waligomea bei mpya kati ya Sh1,900 mpaka Sh2,700 kwa kilo ikiwa ni anguko la kutoka wastani wa Sh4,000 kwa kilo msimu uliopita.

Kutokana na hali hiyo, mbunge wa upinzani na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ambaye amekuwa mwiba kwa serikali ya Magufuli amewaambia waandishi kuwa serikali haiwezi kukwepa lawama.
"Badala ya Serikali kulichukulia zao la korosho kama la kimkakati imekuwa haisikii, haielewi, na sasa imeharibu kuku anayetaga mayai ya dhahabu katika nchi yetu," amesema.
Jana hiyo hiyo Rais Magufuli alifanya kikao na wanunuzi wakuu wa zao hilo na kuwaeleza kuwa serikali inaunga mkono msimamo wa wakulima.
Magufuli alienda mbali kwa kusema serikali yake ipo radhi kuzinunua korosho zote kwa bei inayowafaa wakulima na kuziuza katika masoko ya kimataifa nchini Marekani na Uchina.
"…nipo tayari hata kutumia majeshi yetu kununua korosho na tutatafuta masoko ya uhakika ili tuuze kwa bei nzuri" amesisitiza Rais Magufuli.
Hata hivyo, wafanyabiashara hao wamekubali kununua korosho kwa bei isiyopungua shilingi 3,000. Serikali pia imekubali kwa upande wake kuondosha baadhi ya tozo na vikwazo vilivyopelekea wafanyabiashara kushusha bei.
Korosho
Zao la korosho ni tegemeo kuu la uchumi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania

Awali ilikuwa marufuku kwa korosho kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kusafirishwa kupitia bandari nyengine isipokuwa ya Mtwara lakini serikali sasa imeruhusu kutumika kwa bandari ya Dar es Salaam pia.
Kutoka bandari ya Dar, korosho husafirishwa kwa Sh47 kwa kilo kwa kutumia meli ambazo zimeleta mizigo mingine ikilinganishwa na bandari ya Mtwara ambako kilo moja inasafirishwa kwa shilingi 203/- kwa kutumia meli zinazokodiwa kwa ajili ya kubeba korosho tu.
Mapema mwezi Mwezi Juni mwaka huu kulikuwa na mnyukano bungeni ambapo wabunge bila kujali tofauti zao za kisiasa walikuwa wakiyapinga mapendekezo ya serikali katika Sheria ya Fedha wa mwaka 2018 kwa kuchukua asilimia 100 ya tozo za mauzo ya korosho nje ya nchi (Export levy) kupelekwa mfuko mkuu wa fedha za serikali.
Awali, asilimia 65 ya tozo hiyo ilikuwa ianenda kwenye mfuko wa zao hilo na baadae kurejeshwa kwa wakulima kupitia pembejeo. Hoja ya wabunge wakiongozwa na kamati ya bajeti ilikuwa, hatua ya kuchukua fedha zote ingeleta athari kubwa kwa maendeleo ya zao hilo na wakulima wake.

Mjadala ukawa mkali lakini hoja ya serikali ikapita. Baadae, Rai John Magufuli akasema hakupendezwa na namna ya wabunge wa CCM hususani wa mikoa ya kusini kwa namna walivyolijadili suala hilo, na akatishia kuwa laiti wangeliandamana basi angetuma askari wawaadhibu.
Baadhi ya wakosoaji akiwemo Zitto wanahusianisha kinachoendelea kwenye anguko la bei na hatua ya serikali ya kuchukua fedha zote za tozo za mauzo ya korosho nje ya nchi.
"Mnaweza kuona fedha za kigeni tunazoenda kupoteza kwa uamuzi wa Serikali kuchukua fedha zote za export levy (ushuru wa forodha) badala ya kupeleka zinakostahili," amesema Zitto.
Msimu wa mwaka jana, serikali ya Tanzania iliingiza kiasi cha dola 209 milioni za Marekani kutokana na zao la korosho.

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...