Kampuni moja ya Uchina imetangaza mpango wake wa kubuni ''mwezi bandia" utakaoangaza miji usiku.
Kwa
mujibu wa gazeti la kitaifa la People's Daily, maafisa katika taasisi
ya kibinafsi ya masuala ya anga za juu iliyoko mjini Chengdu inataka
kuzindua "kituo cha satellite kitakachoangaza" ulimwengu.Mradi huo unatarajiwa kuzindiluwa ifikapo mwaka 2020, ambayo pia itakua na mwangaza wa haliya juu utakaochukua nafasi ya taa za barabarani.
Mpango huo umevutia hisia mbali mbali kutoka kwa wanasayansi ambao wanahoji uwezekeno wa kufikiwa kwa mpango huo huku wengine wakiukejeli.
Tunafahamu nini kuhusiana na mradi huu?
Hakuna mengi yaliyoangaaziwa kuhusiana na mradi wenyewe - taarifa zilizotolewa kwa umma pia zinakinzana.
Gazeti la People's Daily iliangzaia mradi huo kwa mara ya kwanza wiki iliyopita.
Gazeti hilo lilimnukuu mwenyekiti wa Taasisi ya mambo ya anga za mbali, Wu Chunfeng aliyegusia mpango huo.
Bwana Wu amesema mradi huo mpya umekua ukifanyiwa majaribio kwa miaka kadhaa sasa na kwamba teknolojia hiyo iko tayari kuzinduliwa ifikapo mwaka 2020.
Haijabainika ikiwa mradi huo umeidhinishwa rasmi na serikali.
Mwezi bandia utafanya vipi kazi?
Kwa mujibu wa gazeti la kitaifa la Uchina mwezi huo utafanya kazi kama kioo ambayo itakua ikielekeza mwangaza wa jua duniani
Utakua unazunguka karibu kilo mita 500- sawa na urefu wa kituo cha kimataifa cha angani.
Mzunguko wa mwezi duniani unakadirika kuwa kilo mita 380,000.
Ripoti hiyo haijatoa maelezo yoyote kuhusu muonekano wa mwezi huo bandia.
Bwana Wu amesema utakua ukileta mwangaza wa jua katika eneo 10km na 80km na utakua na unaangaza mara nane zaidi ya mwezi wa ukweli.
Wu anasema mwangaza wa mwezi huo bandia utadhibitiwa.
Maafisa wa taasisi ya Chengdu wanasema mwangaza huo utadhibitiwa ili kupunguza gharama.
Pia wanasema mwangaza wa mwezi bandia huenda ikawa gharama nafuu kuliko malipo ya taa za barabarani.
Dr Matteo Ceriotti, mhadhiri wa somo la uhandisi wa angaa za mbali katika chuo kikuu cha Glasgow, ameimbia BBC "Nadhani huu ni mfano wa uwekezaji,"
"Umeme unaotumika usiku ni ghali mno kwa hivyo kukipatikana mwangaza mbadala kwa miaka 15 utachangia pakubwa kuimarisha uchumi."
Lakini hilo linawezekana?
Kisayansi kuna uwezekani asema Dr Ceriotti.
Hata hivyo ili kufikia lengo lake , huo mwezi bandia lazima uwe unazunguka maisha jua ya Chengdu - katika eneo ambalo ni dogo ukilinganisha na mduara wa dunia kutoka angani.
Mradi huu utakua na athari gani kwa mazingira?
Watumiaji wa mitandao wa kijamii nchini Uchina wanamasha.
Baadhi yao wanasema tayari kuna uchafuzi wa mazingira unaotokana na mwangaza katika eneo la Chengdu na miji mingine ya China.
Wengine wanasema mwakaza huo bandia utakua na athari kwa viumbe wengine wadogo dunian.
John Barentine, mkurugenzi wa Sera ya Umma katika Chama cha Kimataifa cha Anga za giza , ameiambia jarida la habari la Forbes.
"Mwezi utaongeza mwangaza wa wakati wa usiku katika jiji ambalo tayari linakabiliwa na mwanga mkali, kwa hivyo hakuna haja ya kuwaongezea matatizo zaidi wakazi wa Chengdu,"
Dr Ceriotti pia amaiambia BBC kuwa endapo mwangaza utakua mkali zaidi huenda "ukaathiri mfumo wa usiku wa maumbile ya dunia haliambayo pia huenda ikawa na athari kwa wanyama".
Pia amesema ikiwa mwangaza huo utakua mdogo hautakua na maana yoyote.
Comments
Post a Comment
Here