Genge la majambazi liliingia katika duka moja kwa nia ya kutaka kuiba.
Mwenye duka akawaambia warudi tena baadaye atakapokua na pesa zaidi, na majambazi hao wakaitikia mwito...Ni tukio ambalo unaweza ukalichukulia kama mzaha, lakini kwa mwenye duka mbelgiji anayeendesha biashara ya kuuza sigara mtandaoni ni tukio la kweli na la kuogofya.
Watu sita waliingia katika duka la Didier viungani mwa mji wa Charleroi wakiwa na mpango wa kumuibia.
Mfanyibiashara huyo aliwaambia wezi hao kurejea dukani hapo mwisho wa siku, wakati atakapokua na pesa nyingi za kuwapatia.
Bila kusita watu hao walirejia kama walivyoagizwa na mwenyeduka badala ya kuwapatia pesa alivyowaahidi wakakamatwa na polisi.
Akizungumza na BBC alisema "Ni tukio la kuchekesha,". " Wamepewa jina la majambazi wajinga zaidi nchini Ubelgiji."
Mwenye duka huyo anasema alitumia muda wa dakika 14 akijaribu kujenga uhusiano mzuri na wezi hao.
Didier anasema kuwa alibishana nao kidogo," "Sikuwapatia kitu chochote, lakini nikawaambia wakirudi baadaye nitakua na kama uero 2,000 ama 3,000."
Wezi hao walikubaliana na mwenye duka na kuondoka.
"Nilipowaarifu maafisa wa polisi, hawakuamini wezi hao wangelirudi."
Lakini ilipofika saa kumi na moja unusu jioni walirudi.
Didier anasema kuwa alimuona mmoja wa wezi hao mlangoni akamwambia bado hajakamilisha biashara ya siku.
Wanaume hao waliporejea saa kumi na mbili na nusu jioni, wakakamtwa na maafisa wa polisi ambao walikua wamejificha ndani ya duka hilo tayari kuwakamata.
Wanaume watano walikamatwa miongoni mwao kijana mdogo
Comments
Post a Comment
Here