Skip to main content

Mwanafunzi ashtakiwa baada ya kumtishia mwalimu silaha bandia

Waziri wa elimu wa Ufaransa Jean-Michel BlanquerMwanafunzi mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kusababisha mtafaruku baada ya picha ya video ikimuonyesha akimtisha mwalimu wake silaha bandia, mjini Paris, waendesha mashtaka wameeleza.
Tukio hilo lilirekodiwa na kuwekwa mitandaoni na mmoja wa wanafunzi wenzake
Mvulana huyo mwenye miaka 15 alisema kuwa alifanya ''mzaha'' na kuongeza kuwa hakujua kama alikuwa akirekodiwa,vyombo vya habari nchini ufaransa vimeripoti.
Mwalimu huyo alipeleka malalamiko yake polisi siku ya Ijumaa.
Mwanafunzi huyo alikwenda polisi siku hiyohiyo akiwa kaongozana na baba yake.
Katika video, alionekana akimnyooshea silaha bandia mwalimu wake, aliyekuwa amekaa kwenye dawati.Alimpigia kelele akimtaka amuorodheshe kuwa alikuwa darasani.
Mwalimu aliendelea kufanya kazi kwenye Kompyuta yake huku akizungumza na wanafunzi.
Gazeti moja jijini Paris limeripoti kuwa mwanafunzi huyo alipandwa na ghadhabu kwa kuwa aliandikwa kwenye orodha kwamba hakuwa darasani baada ya kufika darasani katika shule ya Edouard-Branly akiwa amechelewa.
Tukio hilo limekemewa vikali na waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa,Christophe Castaner.
Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais wa nchi hiyo Emmanuel Macron amesema tukio hilo ''halikubaliki''.
Mkutano wa kujadili namna ya kukomesha vitendo vya ghasia shuleni utafanyika viungani mwa jiji la Paris.
Didier Sablic,amekuwa mwalimu wa shule hiyo kwa miaka 25, ameliambia gazeti la Le Monde kuwa ''hajazoea matukio ya namna hii'' , alisema wanafunzi shuleni hapo hufundishwa ''namna ya kuwasiliana na nidham

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...

Je unayafahamu maajabu ya Ziwa Ngosi Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayozungukwa na vivutio vingi vya utalii na vingine inawezekana hata havitambuliwi na wenyeji. Ziwa Ngosi yawezekana kuwa ni miongoni mwa vivutio hivyo. Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.