Skip to main content

Hong Kong-Zhuhai: Daraja refu zaidi duniani lafunguliwa rasmi, mambo muhimu kulihusu

Picha ya kutoka angani ya daraja la Hong Kong-Zhuhai-Macau Bridge Juni 11, 2018 ZhuhaiRais wa China Xi Jinping amefungua rasmi daraja refu zaidi duniani, ambalo limekuwa likijengwa kwa miaka tisa.
Daraja hilo, ukijumuisha pia barabara zinazolinganisha pamoja, lina urefu wa 55km (maili 34) ana linaunganisha Hong Kong na Macau na jiji la China bara la Zhuhai.
Ujenzi wa daraja hilo umegharimu $20bn (£15.3bn) na umecheleweshwa mara kadha.
Kwa kulinganisha, gharama hiyo ni zaidi ya bajeti ya mwaka huu ya Tanzania ambayo ilikuwa $14.2 bilioni, hata ukaongeza bajeti ya Rwanda ambayo ni $2.7 bilioni haufikii hizo $20bn. Bajeti ya Kenya mwaka huu ni $30.3 bilioni.
Ukatumia mwendo wa kawaida wa kutembea wa 5km kwa saa, basi itakuchukua saa 11 kulivuka daraja hilo ukaamua kutembea.
Ujenzi wake ulikumbwa na wasiwasi mara kadha kuhusu usalama wake.
Maafisa wanasema watu zaidi ya 18 walifariki wakati wa kujengwa kwa daraja hilo.
Rais Xi alihudhuria sherehe ya kuzindua daraja hilo ambayo imefanyika jijini Zhuhai, akiwa pamoja na viongozi wa Hong Kong na Macau.
Magari yataruhusiwa kuanza kulitumia Jumatano.
Nini cha kipekee kuhusu daraja hili?
Linaunganisha miji mitatu muhimu kusini mwa China - Hong Kong, Macau na Zhuhai.
Daraja hilo, ambalo limejengwa kuhimili mitetemeko ya ardhi na vimbunga, ilijengwa kwa kutumia tani 400,000 za chuma, chuma zinazotosha kujenga minara 60 sawa na mnara maarufu wa Eiffel jijini Paris.
Takriban 30km ya urefu wake umepitia baharini kwenye mlango wa Mto Pearl.
Ili kuwezesha meli kupita chini ya daraja hilo, kuna sehemu ya urefu wa 6.7km ambapo daraja hilo linaingia chini ya bahari na kupitia kati ya visiwa viwili vya kujengwa na binadamu na hivyo kuwa kama njia ya chini kwa chini baharini.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Moja kati ya visiwa viwili bandia vilivyojengwa
Maeneo yaliyosalia yanaunganishwa kwa barabara, njia za kuondosha maji na barabara za chini kwa chini kukamilisha kuunganisha kikamilifu miji ya Zhuhai na Hong Kong na daraja hilo.
Aerial view of Hong Kong-Zhuhai-Macau Bridge West Artificial Island
Moja kati ya visiwa viwili bandia vilivyojengwa
 Kwa nini likajengwa?
Ni sehemu ya mpango wa China wa kujenga kinachoitwa Greater Bay Area (Eneo Kubwa la Ghuba), ambalo litajumuisha Hong Kong, Macau na miji mingine tisa kusini mwa China.
Eneo hilo kwa sasa lina wakazi 68 milioni, zaidi ya raia wote wa Tanzania au Kenya pia.
Zamani, mtu kusafiri kati ya Zhuhai na Hong Kong angechukua saa nne kukamilisha safari hiyo. Lakini sasa daraja hilo litapunguza hilo hadi kuwa dakika 30 pekee.
Graphic: Bridge and tunnel cross-section and location map 
Unaruhusiwa kuendesha gari darajani?
La hasa. Ndipo uweze kuendesha gari lako kwenye daraja hilo, unahitaji kibali maalum, ambacho kitakuwa vinatolewa kwa watu kwa vipimo.
Aidha, magari yote yatalipa ada kuruhusiwa kutumia daraja hilo.
Katika hilo halijafunguliwa kutumiw ana magari ya uchukuzi wa umma, hivyo ni mabasi ya kibinafsi ambayo yatakuwa yanawasafirisha watu.
Aidha, hakuna reli inayopitia kwenye daraja hilo.
Maafisa awali walikuwa wamekadiria kwamba magari 9,200 yangekuwa yanalitumia daraja hilo kila siku.
Baadaye walishusha makadirio yao baada ya barabara mpya na miundo mbinu ya usafiri kujengwa eneo hilo.
Watu wanasema nini?
Kumekuwa na ukosoaji mkubwa wa mradi huo.
Daraja hilo lilikuwa limeelezwa na baadhi ya vyombo vya habari kama 'daraja la mauti'.
Watu zaidi ya tisa walikuwa wamefariki upande wa Hong Kong wakati wa kujengwa kwa daraja hilo, na maafisa waliambia idhaa ya Kichina ya BBC kwamba watu tisa walifariki upande wa China.
Mamia ya wafanyakazi walijeruhiwa pia wakati wa ujenzi wa daraja hilo.
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Watu 18 walifariki wakati wa ujenzi wa daraja hilo
Kumekuwa pia na wasiwasi kuhusu athari zake kwa mazingira.
Makundi ya kutetea uhifadhi wa mazingira yanasema mradi huo huenda umeathiri sana viumbe wa baharini, ikiwa ni pamoja na pomboo weupe wa China ambao huwa nadra sana kupatikana.
Idadi ya pomboo wanaoonekana katika bahari ya Hong Kong wamepungua kutoka 148 hadi 47 katika miaka 10 iliyopita, na kwa mujibu wa tawi la Hong Kong la shirika la World Wide Fund for Nature (WWF) hakuna pomboo aliyeonekana karibu na daraja hilo.
"Mradi huu umefanya madhara makubwa sana kwa bahari," alisema Samantha Lee, Mkurugenzi msaidizi wa Uhifadhi wa Bahari katika WWF.
"Nina wasiwasi kwamba idadi hii haitaongezeka tena."
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Itakuwa nadra sana kuwaona pomboo weupe wa Kichina baada ya kujengwa kwa daraja hilo
Litaweza kulipia gharama?
Kwa pamoja, daraja hilo na barabara zinazoliunganisha na miundo mbinu mingine, pamoja na visiwa bandia vilivyojengwa baharini viligharimu $20bn. Daraja kuu lenyewe liligharimu $6.92bn.
Maafisa wa serikali nchini China wanasema daraja hilo litachangia kuuzalishia uchumi wa China yuan trilioni 10 ($1.44tn; £1tn), lakini mmoja wa wabunge Hong Kong ametilia shaka hilo.
"Sina uhakika kwamba daraja hilo linaweza kujiendeleza kwa gharama iwapo si magari mengi yatakuwa yanalitumia, alisema Tanya Chana alipozungumza na BBC.
"Nina uhakika kwamba hakuna vile tutaweza kupata tena gharama iliyotumiwa kwa ujenzi."
Kwa mujibu wa makadirio ya Idhaa ya Kichina ya BBC, daraja hilo litakusanya ada ya jumla ya $86m kwa kuwatoza wanaolitumia.
Lakini gharama ya kulisimamia na kufanya ukarabati inatarajiwa kuchukua karibu theluthi moja ya mapato yatakayokusanywa kupitia tozo hiyo.
Wakosoaji wanasema daraja hilo halitakuwa na mafao yoyote kwa uchumi, na wengine wanasema lengo muhimu ni kuhakikisha Hong Kong inaunganishwa na China bara

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...