Skip to main content

Tajiri namba moja duniani(Jeff Bezos) atemana na mkewe(MacKenzie)


Amazon's Jeff Bezos and his wife MacKenzie BezosHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWawili hao wamesema walikwa na maisha ya furaha pamoja

Mmiliki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Amazon Jeff Bezos na mkewe MacKenzie wanatarajiwa kupeana talaka baada ya miaka 25 ya ndoa.
Wawili hao wametoa taarifa ya pamoja kuhusu suala hilo kupitia mtandao wa Twitter siku ya Jumatano.
"Baada ya kipindi kirefu cha mapenzi na kujaribu kutengana, tumeamua kuachana na kuendelea na maisha yetu kama marafiki," wawii hao wamesema kwenye taarifa yao ya pamoja.
Amazon, ambayo imeanzishwa miaka 25 iliyopita wiki hii imeifunika Microsoft na kuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani.
Amazon ina thamani ya dola bilioni 797 baada ya soko la hisa la Marekani kufungwa siku ya Jumatatu baada ya kukua kwa asilimia 3.4 ikiipiku Microsoft ya Bill Gates yenye thamani ya dola bilioni 789.
Bw Bezos, 54, ambaye ni mwanzilishi wa Amazon, ndiye mtu tajiri zaidi ulimwenguni kwa mujibu wa chati ya jarida mashuhuri la biashara la bloomberg, akiwa na utajiri unaokisiwa kufikia dola bilioni 137, akimzidi Bill Gates kwa dola bilioni 45.
Bi MacKenzie Bezos mwenye miaka 48 ni mtunzi wa vitabu, na baadhi ya maandiko yake ni The Testing of Luther Albright (2005) na Traps (2013).
"Tunajihisi ni wenye bahati kwa kufahamiana na tunafurahia miaka yote tuliyokuwa pamoja kwenye ndoa," taarifa ya wawili hao imeeleza.

The couple photographed in 2004Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWawili hao walifunga ndoa mwaka 1993 baada ya kukutana kwenye usaili wa kazi

"Laiti tungelijua kama tungetengana baada ya miaka 25, basi tungelianza upya. Tumekuwa na maisha bora kabisa kama wanandoa na pia tunaona mustakabali mzuri kama wazazi, marafiki na washirika katika miradi na biasha mbali mbali.
"Japo nembo zitabadilika, tutabaki kuwa familia, na tutaendelea kuwa marafiki wa kipekee."
Mwaka jana walianzisha kwa pamoja wakfu uitwao Day One Fund unaolenga kuwasaidia watu wasiokuwa na makao pamoja na kujenga shule za awali kwenye maeneo waishio watu wenye vipato duni.
Wawili hao wana watoto wanne - wavulana watatu na binti mmoja ambaye wamemuasili.
Vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti kuwa Bw Bezos yupo kwenye dimbi la mahaba na mtangazji wa zamani wa runinga ya Fox TV, Bi Lauren Sanchez.
Mtandao wa habari za burudani wa TMZ, ukinukuu vyanzo vilivyo karibu na Bi Ms Sánchez, unadai kuwa wawili hao wamekuwa kwenye mapenzi mpaka mwisho wa mwaka jana.
Mwaka 2013, MacKenzie Bezos aliliambia jarida la Vogue kuwa alikutana na Jeff wakati akimfanyia usaili wa kazi katika wakfu wa Hedge jijini New York.
Wawili hao waliingia katika uchumba miezi mitatu tu toka walipoanza mahusiano na kufunga ndoa muda mfupi baadae mnamo mwaka 1993. after, in 1993.
Mwaka mmoja baadae Jeff akaanzisha Amazon - kama kampuni ya kuuza vitabu reja reja mtandaoni.
Kampuni hiyo imekua toka hapo na kuwa gwiji nambari moja wa biashara ya mtandao duniani.

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...