Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2019

Vimbunga vilivyopewa majina duniani(Kimbunga Kenneth, Matthew, Katrina).

Haki miliki ya picha Umewahi kusikia vimbunga vikiwa na majina ya kushangaza, kilichoitwa Idai kilichosababisha uharibifu mkubwa katika baadhi ya maeneo nchini Msumbiji, Malawi na Zimbabwe mwezi uliopita Machi katika kile ambacho Umoja wa mataifa unasema huenda ni janga baya zaidi la hali ya hewa kuwahi kushuhudiwa kusini mwa Afrika. Matthew ambacho kilikumba maeneo ya Haiti, Jamaica, Jamhuri ya Dominika, Bahamas na baadhi ya majimbo ya Marekani mwezi Oktoba mwaka 2016. Mwezi uliotangulia kulikuwa na kimbunga kingine kilichojulikana kama Hermine ambacho kilisababisha uharibifu mkubwa jimbo la Florida. Lakini kinachokumbukwa sana ni kile kwa jina Katrina ambacho kiliathiri sana majimbo ya Louisiana, Mississippi na Alabama nchini Marekani. Je, vimbunga hivi hupewa vipi majina? Haki miliki ya pich TERS Vimbunga vinavyopewa majina Vimbunga katika maeneo ya bahari ya Atlantiki, maeneo ya Caribbean na Ghuba ya Mexico hupewa majina ya Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa D...

Kulala bila nguo kuna hatari zozote?

Haki miliki ya picha Kila mtu huwa ana namna yake ya kulala ambayo anajiona kuwa yuko huru Takwimu zinaonesha kwamba idadi kubwa ya vijana, na hasa Ulaya, huwa hawavai nguo ya aina yoyote ile wanapolala. Je, kuna madhara au manufaa? Unafaa kulala bila nguo? Mtaalam wa usingizi Dkt Nerina Ramlakhan ameambia BBC kwamba kuna faida ambazo mtu anaweza kuzipata akivaa nguo za kulalia wakati anapolala. "Kila mtu ana upekee wake na kila mtu ana namna yake ya kulala ambayo anaona huwa inampa uhuru au raha. Kuna baadhi ya watu hawapendi kulala bila nguo huku wengine huwa hawajali kabisa," Dkt Ramlakhan. Anaongeza kwamba kila mtu huwa anahitaji kiwango cha joto ambacho kwake kinamfanya aweze kulala vizuri, na kwa kawaida huwa chini kidogo ya kiwango cha joto mwilini. Anashauri kuwa kama unavaa nguo wakati wa kulala au huvai ni vyema kutumia kitanda chenye godoro zuri, na vilevile vazi zuri la kulalia ni lile la nguo nyepesi. Je ,  kuna ubaya wa kulala bila nguo ? Dkt. R...

Umuhimu kupata usingizi wa kutosha

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Mtu huyu anakosa usingizi Mambo yanayozushwa kuhusu usingizi yanaharibu afya zetu na hali zetu, pia kufupisha maisha yetu, wanasema watafiti. Watafiti katika Chuo kikuu New York walitafiti kuhusu suala la usingizi. Kisha kisayansi wakatafutia ushahidi. Wana matumaini kuwa tabia ambazo tunaziona za kawaida na tunazoamini kuwa zitatusaidia kwa afya ya miili na akili ni imani tu. Imani ya  1 -  Unaweza kuwa sawa hata ukilala kwa muda wa chini ya saa tano Hii ni imani ambayo haiwezi kuondoka Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher alikua anapata saa nne za kulala usiku.Kansela wa Ujerumani. Angela Merkel alikua na madai kama hayo, akibadili saa zake za kulala kuwa saa za ziada kufanya kazi ofisini . Lakini watafiti walisema kuamini kuwa kufunga macho kwa kipindi cha chini ya saa tano ni jambo zuri kwa afya, ni moja kati ya imani mbaya iliyo hatari kwa afya. ''Tuna ushahidi thabiti unaoonyesha kuwa kulala...

Itambue miji yenye gharama kubwa na gharama za chini kuishi duniani

Haki miliki ya pich  IMAGES Paris ndio mji ulio na gharama kubwa zaidi duniani, ukiandamana na Hong Kong na Singapore. Ni mara ya kwanza miji mitatu imekuwa katika nafasi sawa juu katika historia ya miaka 30 ya utafiti wa kila mwaka wa uchumi - Economist Intelligence Unit, inayolinganisha gharama katika miji 133 duniani. Mji mkuu wa Ufaransa - ulio katika nafasi ya pili kwa gharam kubwa ya maisha mwaka jana - ndio nchi ya pekee ya Ulaya iliopo katika nafasi ya juu mwaka huu. Utafiti huo umelinganisha bei za bidhaa za kawaida kama mkate katika miji 133. Alafu inafuatilia iwapo bei hizo zimepanda au zimeshuka kwa kuzilinganisha na gharama ya maisha katika mji wa New York, Marekani. Mithilisho Mhariri wa ripoti hiyo Roxana Slavcheva amesema Paris umekuwa mojwapo ya miji kumi iliyo na gharama kubwa kuishi tangu 2003. "Ni pombe tu, usafiri na tumbaku ulio na gharama nafuu ikilinganihswa na mataifa mengine ya Ulaya," amesema. Kiwango cha gharama kwa mwanamke kuka...

Je Familia ya Kardashian imetoa wapi mamilioni ya dola?

Haki miliki ya pich  IMAGES Image caption Kutoka kushoto, Kris Jenner, Khloe Kardashian, Kendall Jenner, Kourtney Kardashian, Kim Kardashian West, North West, Caitlyn Jenner na Kylie Jenner Kipindi cha Televisheni kinachoonesha maihsa ya uhalisi 'Keeping up with the Kardashians' kimeanza upya kwa msimu wa 16, kumaanisha mvutano na malumbano ya familia hiyo yanaywekwa parwanja kwa mara nyingine. Kipindi hicho kimekuwa kikipeperushwa kwa muda unaozidi muongo mmoja sasa, huku utajiri wa familia huo ukikuwa kwa kadri ya miaka ya kipindi hicho. Kylie Jenner - ambaye wakati kipindi hicho ha TV kilipoanza alikuwa na miaka 9 - sasa ana miaka 21 na ni bilionea. Akiwa na utajiri unaokadiriwa $1bn (£760m), kwa mujibu wa jarida la Forbes, mwanadada huyo mmiliki wa kampuni ya vipodozi ndiye aliye tajiri zaidi kati ya wanfamailia nzima ya Kardashian clan, inayoongozwa na kusimamiwa na mama Kris Jenner. Hatahivyo, ndugu zake wengine pia sio kwamba hawajiwezi. Kim Kardashian We...