Skip to main content

Posts

Tajiri namba moja duniani(Jeff Bezos) atemana na mkewe(MacKenzie)

Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Wawili hao wamesema walikwa na maisha ya furaha pamoja Mmiliki na Afisa Mtendaji Mkuu wa Amazon Jeff Bezos na mkewe MacKenzie wanatarajiwa kupeana talaka baada ya miaka 25 ya ndoa. Wawili hao wametoa taarifa ya pamoja kuhusu suala hilo kupitia mtandao wa Twitter siku ya Jumatano. "Baada ya kipindi kirefu cha mapenzi na kujaribu kutengana, tumeamua kuachana na kuendelea na maisha yetu kama marafiki," wawii hao wamesema kwenye taarifa yao ya pamoja. Amazon, ambayo imeanzishwa miaka 25 iliyopita wiki hii imeifunika Microsoft na kuwa kampuni yenye thamani kubwa zaidi duniani. Amazon ina thamani ya dola bilioni 797 baada ya soko la hisa la Marekani kufungwa siku ya Jumatatu baada ya kukua kwa asilimia 3.4 ikiipiku Microsoft ya Bill Gates yenye thamani ya dola bilioni 789. Bw Bezos, 54, ambaye ni mwanzilishi wa Amazon, ndiye mtu tajiri zaidi ulimwenguni  kwa mujibu wa chati ya jarida mashuhuri la biashara la bloomberg , akiwa ...

Floyd Mayweather ampiga 'knockout' mara tatu Tenshin Nasukawa na kushinda katika raundi ya kwanza

Haki miliki ya picha AFP Image caption Mayweather aikuwa akitabasamu alipombwaga mpinzani wake Nasukawa Floyd Mayweather alihitaji sekunde 140 pekee kumshinda mpinzani wake wa Japan Tenshin Nasukawa katika pigano la maonyesho lililokuwa na thamani ya dola $9m. Bingwa huyo mara tano wa zamani Mayweather mwenye umri wa miaka 41 alikuwa akitabasamu wakati wa pigano hilo la muda mfupi mjini Tokyo alipombwaga mara tatu mpinzani wake mwenye umri wa miaka 20. Pigano hilo la raundi tatu lilimalizika huku Nasukawa akibubujikwa na machozi baada ya kikosi chake kurusha kitambaa cheupe ndani ya ulingo kikitaka pigano kusitishwa. Licha ya kurudi katika pigano hilo Mayweather alisema yeye amestaafu ndondi za kulipwa. ''Ni hatua ya kuburudisha tu, tulifurahia sana , alisema raia huyo wa Marekani ambaye alimshinda bingwa wa UFC Conor McGregor katika pigano la masumbwi mnamo mwezi Agosti 2017. ''Walitaka pigano hili kufanyika nchini Japan hivyobasi nikasema kwa nini lisifanyi...

STEVE CHEN: YOU TUBE co founder

Steve Chen 陳 士 駿 Chen in 2007 Born Steven Shih Chen August 18, 1978 (age 40) Taipei , Taiwan Residence San Francisco , California , U.S. Alma mater University of Illinois at Urbana-Champaign Occupation Co-Founder of AVOS Known for Co-Founder of YouTube Net worth $300 million Spouse(s) Park Ji-hyun (Jamie Chen) Children 2 Steven Shih Chen ( traditional Chinese : 陳 士 駿 ; simplified Chinese : 陈 士 骏 ; pinyin : Chén Shìjùn ; born August 18, 1978) is an American Internet entrepreneur . He is one of the co-founders and previous chief technology officer of the video-sharing website YouTube . After having co-founded the company AVOS Systems, Inc. and built the video-sharing app MixBit , [1] he joined Google Ventures in 2014. [2] Early years and education Chen was born in Taipei , Taiwan . When he was fifteen, he and his family immigrated to the United States [3] and settled in Prospect Heights, Illinois . [4] He went to River Trai...

Grace Mugabe anashutumiwa kumjeruhi mwanamitindo nchini Afrika Kusini

  Waendesha mashtaka nchini Afrika Kusini wametoa waranti ya kukamatwa kwa mke wa Rais wa zamani wa Zimbabwe,Grace Mugabe, kutokana na tuhuma za kumshambulia mwanamitindo mwaka 2017, Polisi wameeleza. Hatua hiyo imekuja baada ya mahakama kuibatilisha kinga yake ya kidiplomasia mwezi Julai. Serikali ya Afrika Kusini ilikosolewa kwa kuruhusu Bibi Mugabe kuondoka nchini humo baada ya mashambulizi. Gabriella Engels alimshutumu kwa kumpiga katika chumba cha hoteli mjini Johannesburg. Msemaji wa polisi,Vishnu Naidoo amesema ''Siwezi kuthibitisha kuwa hati ya kumkamata Grace Mugabe ilitolewa Alhamisi iliyopita''. Alisema polisi wanatafuta usaidizi kutoka idara ya Interpol kufanyia kazi waranti hiyo. Haijafahamika kwa nini ripoti kuhusu waranti hiyo ilicheleweshwa na hakuna tamko lolote lililotolewa na Bibi Mugabe au mamlaka za Zimbabwe. Familia ya Mugabe inamiliki mali nchini Afrika Kusini Tukio la mashambulizi dhidi ya mwanamitindo lilitokea miezi mitatu ...

Dermophis donaldtrumpi: Kiumbe anayeishi baharini na nchi kavu apewa jina Donald Trump

  EnviroBuild, ndio kampuni iliyopata haki ya kumpa kiumbe huyo jina, iliongeza nywele bandia kwenye kiumbe huyo jambo lililomfanya kuwa na muonekano unaokaribiana na wa Trump. Kiumbe anayeweza kuishi baharini na katika nchi kavu amepewa jina la Rais wa Marekani Donald Trump, ingawa huenda kiongozi huyo asitake kuhusishwa na kiumbe huyo kutokana na sifa zake. Amfibia huyo huwa anafukia na kuficha kichwa chake mchangani anapokabiliwa na hatari, jambo ambalo pengine limewashawishi wahusika kumpa kiumbe huyo jina la Trump kutokana na kiongozi huyo kukana kwamba shughuli za viwanda na za kibinadamu zinachangia mabadiliko ya tabia nchi. Kiumbe huyo pia ni kipofu, hawezi kuona. Mnyama huyo ambaye amepewa jina Dermophis donaldtrumpi , aligunduliwa katika eneo la Panama, na alipewa jina hilo na mkuu wa kampuni ya EnviroBuild ambaye alikuwa amelipa $25,000 (£19,800) kwenye mnada kupata fursa ya kumpa jina kiumbe huyo. K...

BASATA: Tuna mamlaka na uwezo wa kuwazuia Diamond Platnumz na Rayvanny kutumbuiza nje ya Tanzania

Baraza la Sanaa la Taifa nchini Tanzania (BASATA) limetetea hatua yake ya kuwapiga marufuku wanamuziki Diamond Platnumz na Rayvanny dhidi ya kufanya tamasha zozote kwa muda usiojulikana. Basata walitangaza uamuzi huo Jumanne wakisema hatua yao ilitokana na wawili hao kutofuata maagizo waliyopewa na baraza hilo wimbo wao wa Mwanza ulipopigwa marufuku Novemba. Wasanii hao wawili walikuwa awali wametakiwa kuuondoa wimbo wao kwa jina 'Mwanza' kutoka kwenye mitandao ya kijamii, lakini wimbo huo umeendelea kuwepo kwenye YouTube na wamekuwa wakiucheza kwenye tamasha mbalimbali. Kadhalika, Diamond ambaye jina lake halisi ni Nasibu Abdul Juma Issaack, Rayvanny ambaye jina lake halisi ni Raymond Shaban Mwakyusa na Wasafi Limited walikuwa wametakiwa kila mmoja kulipa faini ya shilingi milioni tatu za Tanzania kabla ya siku 14 kupita "Baraza limefikia maamuzi ya kuwafungia rasmi kutokana na wasanii hawa kuendelea kuonyesha dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka zinazosimamia ...

Fastjet: Shirika la ndege lapewa makataa kujieleza kwa nini wasifungiwe Tanzania

Shirika la ndege la Fastjet Airlines Limited maarufu kama Fastjet Tanzania limepewa makataa ya siku 28 kueleza sababu zinazoweza kuzuialisifungiwe kuendelea kuhudu Tanzania. Kwa mijibu wa Mamlaka ya Safari za Anga Tanzania, shirika la ndege la Fastjet limekosa sifa ya leseni ya usafiri wa anga kwa sababu halina ndege zozote kwa sasa. TCAA imesema ilitoa notice ya siku 28 ya kulitaka shirika hilo lisitishe mauzo kwa abiria. Na limeamuru shirika hilo kurejesha pesa kwa abiria hao au kuwatafutia usafiri katika mashirika mengine. Mamlaka hiyo pia imeamuru waliopata hasara wafidiwe kwa mujibu wa sheria, na watoe mpango mkakati kwa nini wasifutiwe leseni ndani ya siku 28, pia ikitokea shirika hilo limefungwa basi walipe stahiki za wafanyakazi. Fastjet tayari wametangaza kusitisha safari zake zote za mwezi Desemba na mwezi Januari. Na wameahidi kurejesha nauli za abiria wote kuanzia tarehe 20 mwezi de...