Skip to main content

‘Wanawake wanaoamka mapema wapo kwenye uwezekano mdogo kupata saratani ya matiti

woman waking up happy
Wanawake wanaoamka mapema wapo katika uwezekano mdogo wa kupata saratani ya matiti, kwa mujibu wa watafiti nchini Uingereza.
Kundi la wanasayansi kutoka chuo cha Briton wanasema sababu ya uhusiano wa muda wa kuamka na hatari ya saratani bado inahitaji kufahamika.
Wanaongeza kuwa ugunduzi huo ni muhimu kwa kuwa kuwa unamuathiri mwanamke.

Saa ya mwili

Kila mtu ana kile kinachofahamika kama saa ya mwili ambayo inaonyesha jinsi mwili unafanya kwa saa 24. Hi inajulikana kwa lugha ya kiingereza kama circadian rhythm.
Inaathiri kila kitu kutokana muda tunaolala, hisia zetu na hata hatari yetu ya kupatwa na mshutuko wa moyo.
Lakini sio kila saa ya mwili ya kila mtu inayoonyesha muda ulio sawa.
Watu wa asubuhi au "larks" huamka mapema, hufanya kazi mapema na huchoka mapema.
Watu wa jioni au "owls" huwa na wakati mgumu kuamka mapema, huwa wa mazao baadaye jioni na hupenda kulala wakiwa wamechelewa.
Lark or owl image

Hili huwa na athari kwa ugonjwa wa saratani?

Watafii wanafikia hivyo. Walitumia njia moja ya kuchambua data inayojulikana kama Mendelian randomisation.
Walichunguza DNA inayoonyesha ikiwa sisi ni watu wa asubuhi au watu wa jioni.
Walitumia taarifa hizo kuwafanyia majaribio wanawake 180,000 nchini Uingereza.
Walionyesha kuwa watu walio na jenetiki za kurauka mapema walikuwa hatari ya chini ya kupatwa na saratani ya matiti kuliko wale walio na tabia za kutomka asubuhi.

Athari hii ni kubwa kwa kiwango gani?

Karibu mwanamke mmoja kati ya saba hupata saratani ya matiti nchini Uingereza katika maisha yake.
Lakini uchunguzi huu uliangazia kiaisi kidogo cha maisha ya mwanamke.
Katika kipidi hicho ilibainika watu wawili katika ya watu 100 wasiorauka mapema walipata saratani ya matiti ikilinganishwa na mmoja kati ya watu 100 waliomka mapema.
Umri na historia ya familia ni baadhi ya masuala yanayochangia mtu kuwa na saratani.

Je usingizi mnono unaweza kuzuia saratani?

Usingizi mnonoHaki miliki ya picha
Si rahisi namna hiyo.
Dkt Richmond amesema bado ni mapema kuwapa ushauri wa moja kwa moja wanawake juu ya suala hilo.
"Bado tunahitaji kujua kwanini mtu anayechelewa kuamka kuwa yupo kwenye hatari kuliko wa asubuhi…Inabidi tufumbue fumbo hilo kwanza."
Bado kuna maswali mengi ambayo hayajapata majibu juu ya uhusiano wa kuwahi ama kuchelewa kuamka na uwezekano wa kupata saratani.

Je watafiti wapo sawa?

Sayansi kwa kawaida haitoi majibu ya uhakika kwa asilimia 100, lakini utafiti huu tayari unamashiko.
Shirika la Afya Duniani (WHO) katika moja ya tafiti zao wameonesha kuwa kujinyima usingizi ama kuusumbua mwili kutoka usingizini mapema kuna uhusiano na hatari ya kupata saratani.
Dkt Richard Berks kutoka taasisi ya Breast Cancer Now, amesema: "Matokeo ya utafiti huu yanaongeza ushahidi uliokuwepo juu ya uhusiano wa usingizi na kansa ya matiti, lakini utafiti zaidi unahitajika ili kupata majibu ya baadhi ya maswali ambayo yanagonga vichwa."

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.