Skip to main content

Chika Okafor, Onyeka Ufere na Ogechi Babalola: Dada watatu wa Nigeria walioshika mimba wakati mmoja Marekani

Pregnant Sisters
Huwa ni furaha kwa mwanamke kushika mimba na kujawa na matumaini ya kujifungua, na huwa kawaida kwa dada kumfichulia dadaki habari punde anapothibitisha.
Ogechi Babalola alikuwa na furaha kama hiyo alipogundua kwamba alikuwa ameshika mimba na angejifungua kifungua mimba wake.
Lakini alipokwenda kuwafichulia dada zake, kila mmoja aligundua kwamba alikuwa anabeba mimba.
Watatu hao, waliozaliwa Nigeria ingawa kwa sasa wanaishi Marekani, walipigwa picha kwa pamoja, wakiwa wajawazito, picha ambazo zimewavutia watu si haba mtandaoni - wengi wakifurahia pamoja nao.
Kwanza Ongechi alikwenda kwa Chika Okafor na kumfichulia habari.
Onyeka Ufere, 30, alipofahamishwa, naye akawafahamisha kwamba naye alikuwa mjamzito.
Mmoja wao, Chika Okafor ndiye aliyepakia picha hizo kwenye mtandao wa Instagram na kuongeza ujumbe: "Kama wanifahamu vyema, basi wafahamu kwamba huwa nawapenda sana dada zangu. Nimekuwa nikigawana nao karibu kila kitu (mavazi, walimu, wazazi, chakula). Sasa tutakuwa pamoja kwenye safari hii ya kusisimua ya kuwa mama. Mungu na wakati wake, ni kama mwujiza. Singefikiria hata wakati mmoja kwamba hili lingetokea."
Wameambia chombo kimoja cha habari kwamba hawakufahamu jinsi kisa chao kilivyokuwa cha kipekee.
Wote wameolewa, na wanatarajia kujifungua watoto wao wakiwa wameachana kwa wiki kadha tu.
"Kwangu na dadangu Chika, ulikuwa ni wakati wetu wa kwanza kushika mimba, na kwa hivyo wazo la kufanya hivi tukiwa peke yetu lilikuwa linatutia wasiwasi. Onyeka amepitia hili awali, ambapo alijaliwa watoto pacha," Babalola aliambia Yahoo Lifestyle.
Anasema hakuna kule kulalamika, kucheka na kusumbuka na kutokwa na machozi kwani katika kila analolipitia, anafahamu kwamba kuna mwenzake ambaye anapitia kitu sawa na hicho.
Babalola, 26, na Okafor, 27, wanatarajia kujifungua watoto wavulana.
Ufere, 30, anatarajia kujifungua watoto wengine pacha, lakini bado hajabaini jinsia yao.
Anatarajia kufahamu hilo Desemba.
Wanawake hao waliozaliwa Nigeria waliamua kupigwa picha za pamoja wakiwa wajawazito walipofahamu kwmaba dada yao mdogo alikuwa azuru California, jimbo walilokulia. Kwa sasa anaishi Atlanta.
Huo ulikuwa wakati wa kwanza kwao kukutana wakiwa wajawazito na hivyo wakaamua kuwa na kumbukumbu.
"Kwani ni mara ngapi mtapata tena fursa ya kuwa wajawazito kwa pamoja? Ni baraka ambayo lazima tuinakili," Okafor aliambia Yahoo Lifestyle.
Picha zilipigwa na rafiki yao Cynthia Onyejiji.
Dada hao wanatumai kwamba uhusiano wao wa karibu utaigwa na watoto wao.

Comments

Post a Comment

Here

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...