![Ukishindwa kufikia malengo ya kibiashara , basi mende kama huyo halali yako](https://ichef.bbci.co.uk/news/660/cpsprodpb/181AA/production/_104203789__104201463_sciencephotolibrary003355043.jpg)
Polisi wamechukua hatua baada ya video kuowaonesha wafanyakazi hao wakichapwa kwa mkanda na kunywa kitu kioevu chenye rangi ya njano.
Mameneja watatu wamehukumiwa kifungo jela kati ya miaka mitano na kumi kutokana na tukio hilo, linaarifu gazeti la Morning Post limearifu.
Video hiyo imekuwa maarufu mitandaoni na watu kutumiana kwa wingi kwenye mitandao nchini China na tovuti mbali mbali ikiwemo tovuti ya Weibo iliyoweka video inayomuonesha muajiri wa kiume akiwa amesimama katikati ya mduara akipigwa mjeledi.
![Video hiyo haraka sana ikawekwa kwenye tovuti ya Weibo](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/2602/production/_104203790__104201471_0293b03e-9c2c-41cc-9c25-6c0a4aa7d79a.jpg)
Wafanyakazi wengine, inaarifiwa kuwa ukiwa ni muajiriwa katika kampuni ya ukarabati majengo katika mji wa Guizhou, si ajabu kuonekana ukinywa kimiminika chenye rangi ya manjano kilichowekwa katika kijikombe cha plastiki huku ukiwa umebinya pua yako .
Ujumbe ulionaswa kwa picha uliosemekana kutoka kwa wasimamizi wa mgahawa huo, zilijaa vitisho kwa wafanyakazi kwamba watalazimika kula mende kutokana na uwajibikaji wao mdogo kikazi.
Kwa muujibu wa vyombo wa habari nchini humo, aina nyingine ya aibu na adhabu katika kampuni hiyo ni pamoja na kunywa maji ya kutawaza yaliyoko chooni ama maji ya siki na kunyoa vipara vichwa vyao.
![picha inayoonekana na vijikombe vidogo vili oneshwa kwenye mitandao ya jamii nchini humo na kuelezwa kuwa kimiminika hicho ni mkojo](https://ichef.bbci.co.uk/news/624/cpsprodpb/15A9A/production/_104203788__104201469_03a56f79-b3dc-4952-a685-7d93e4b0821d.jpg)
picha inayoonekana na vijikombe vidogo vili oneshwa kwenye mitandao ya jamii nchini humo na kuelezwa kuwa kimiminika hicho ni mkojo
Polisi katika kata ya Zunyi waliwatia mbaroni mameneja watatu na baadaye kufuwahukumu kifungo cha maisha jela.
Katika siku za hivi karibu imekuwa ni mastaajabu kwa makampuni ya kichina kutumia adhabu kama hizo, kuadhirisha ama kuwatia moyo wafanyakazi wao.
Taarifa za hivi karibuni zinaarifu kuwa kumekuwa na mifano ya kesi kama hizo kwa wafanyakazi kupigana makofi wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuongeza ari kazini, na wafanyakazi kulazimishwa kutambaa barabarani ama kubusu mapipa ya takataka kama adhabu au kuongeza mshikamano kazi.
Kampuni hiyo pia inaarifiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kwa muda wa miezi miwili iliyopita, na wafanyakazi walikuwa na hofu ya kuzungumzia suala hilo kwa kuhofia kupoteza malipo yao enapo pia wataacha kazi
noumaaa
ReplyDeletepoapoa jombaaaa
ReplyDeleteyechu wanyumbaniii!!!
ReplyDelete