Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2018

Rais Magufuli atema cheche anguko la bei ya korosho Tanzania

Panda shuka za zao la korosho nchini Tanzania zimemvuta Rais John Pombe Magufuli na sasa ametishia tena kuchukua hatua kali. Siku chache zilizopita msimu mpya wa mauzo ya zao la korosho ulifunguliwa huku bei ya zao hilo zikishuka maradufu. Korosho ndio chanzo kikuu cha fedha na tegemeo la kiuchumi kwa wakazi wa mikoa ya kusini mwa Tanzania. Wakaazi hao kutokana na unyeti wa sekta hiyo waligomea bei mpya kati ya Sh1,900 mpaka Sh2,700 kwa kilo ikiwa ni anguko la kutoka wastani wa Sh4,000 kwa kilo msimu uliopita. Kutokana na hali hiyo, mbunge wa upinzani na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ambaye amekuwa mwiba kwa serikali ya Magufuli amewaambia waandishi kuwa serikali haiwezi kukwepa lawama. "Badala ya Serikali kulichukulia zao la korosho kama la kimkakati imekuwa haisikii, haielewi, na sasa imeharibu kuku anayetaga mayai ya dhahabu katika nchi yetu," amesema. Jana hiyo hiyo Rais Magufuli alifanya kikao na wanunuzi wakuu wa zao hilo na kuwaeleza kuwa serikal...

Mwanafunzi ashtakiwa baada ya kumtishia mwalimu silaha bandia

Mwanafunzi mmoja ameshtakiwa kwa kosa la kusababisha mtafaruku baada ya picha ya video ikimuonyesha akimtisha mwalimu wake silaha bandia, mjini Paris, waendesha mashtaka wameeleza. Tukio hilo lilirekodiwa na kuwekwa mitandaoni na mmoja wa wanafunzi wenzake Mvulana huyo mwenye miaka 15 alisema kuwa alifanya ''mzaha'' na kuongeza kuwa hakujua kama alikuwa akirekodiwa,vyombo vya habari nchini ufaransa vimeripoti. Mwalimu huyo alipeleka malalamiko yake polisi siku ya Ijumaa. Mwanafunzi huyo alikwenda polisi siku hiyohiyo akiwa kaongozana na baba yake. Katika video, alionekana akimnyooshea silaha bandia mwalimu wake, aliyekuwa amekaa kwenye dawati.Alimpigia kelele akimtaka amuorodheshe kuwa alikuwa darasani. Mwalimu aliendelea kufanya kazi kwenye Kompyuta yake huku akizungumza na wanafunzi. Gazeti moja jijini Paris limeripoti kuwa mwanafunzi huyo alipandwa na ghadhabu kwa...

Je unayafahamu maajabu ya Ziwa Ngosi Tanzania

Tanzania ni miongoni mwa nchi barani Afrika inayozungukwa na vivutio vingi vya utalii na vingine inawezekana hata havitambuliwi na wenyeji. Ziwa Ngosi yawezekana kuwa ni miongoni mwa vivutio hivyo. Ziwa hili ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ziwa lingine la kreta lililopo Ethiopia linaakisi muonekano wa bara la Afrika katika upande wa kusini, magharibi, kaskazini na mashariki pamoja na visiwa vyake vya Unguja na Pemba.

Jamal Khashoggi: Mchumba wa mwandishi Khashoggi akataa mwaliko wa Donald Trump

Mchumba wa mwanahabari wa Saudia aliyeuawa Jamal Khashoggi anasema amesusia mwaliko wa rais wa Marekani Donald Trump katika Ikulu ya White House kwa madai kiongozi huyo wa haijaonesha nia ya kutaka kujua ukweli kuhusu mauaji hayo ya kikatili. Hatice Cengiz amekiambia kituo kimoja cha Televisheni nchini Uturuki kwamba mwaliko huo unalenga kubadili maoni ya Wamarekani Khashoggi aliuawa ndani ya ubalozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul wiki tatu zilizopita.   Riyadh imekanusha madai ya kuhusishwa kwa familia ya kifalme katika mauaji hayo na badala yake imelaumu watu iliyowataja kuwa''maajenti wakatili'' Katika mahojiano ya kusikitisha katika televisheni bi Cengiz alielezea jinsi mchumba wake alivyotoweka baada ya kuingia ubalozi wa Saudia mji...

Mwezi Bandia: China inaweza kuangaza mawingu usiku?

Kampuni moja ya Uchina imetangaza mpango wake wa kubuni ''mwezi bandia" utakaoangaza miji usiku. Kwa mujibu wa gazeti la kitaifa la People's Daily, maafisa katika taasisi ya kibinafsi ya masuala ya anga za juu iliyoko mjini Chengdu inataka kuzindua "kituo cha satellite kitakachoangaza" ulimwengu. Mradi huo unatarajiwa kuzindiluwa ifikapo mwaka 2020, ambayo pia itakua na mwangaza wa haliya juu utakaochukua nafasi ya taa za barabarani. Mpango huo umevutia hisia mbali mbali kutoka kwa wanasayansi ambao wanahoji uwezekeno wa kufikiwa kwa mpango huo huku wengine wakiukejeli. Tunafahamu nini kuhusiana na mradi huu ? Hakuna mengi yaliyoangaaziwa kuhusiana na mradi wenyewe - taarifa zilizotolewa kwa umma pia zinakinzana. Gazeti la People's Daily iliangzaia mradi huo kwa mara ya kwanza wiki iliyopita. Gazeti hilo lilimnukuu mwenyekiti wa Taasisi ya mambo ya anga za mbali, Wu Chunfeng aliyegusia mpango huo. Bwana Wu amesema mradi huo mpya umekua...

Utafiti mpya umebaini kuwa watu warefu zaidi wapo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa Saratani

Utafiti mpya wa kiafya umebaini kuwa watu warefu zaidi wapo katika hatari ya kuwa na ugonjwa wa Saratani. Mwandishi wa ripoti ya utafiti huu Dr Leonard Nunney anasema watu walio katika mazingira ya kupata ugonjwa wa saratani iwapo tu atakuwa na ongezeko la urefu wa kawaida kwa kuanzia sentimita kumi,basi hapo ni jambo la kujiuliza mara mbili. "Iwapo wastani wa wanawake 50 kati ya 500 watapata saratani, wastani huo unabadilika ifikapo kwa wanawake 60 kwa 500 warefu kufikia kimo cha sentimita 178 ambao kwa mjibu wa utafiti huo, wanakuwa katika uwezekano mkubwa wa kupata Saratani''.imebainisha ripoti hiyo. Ripoti ya utafiti huu mpya inakuja huku suala la uvutaji sigara likiendelea kutajwa kuwa chanzo kikubwa cha kupata ugonjwa wa Saratani,sasa kama kimo nacho ni sababu kubwa ya kupata ugonjwa ...

Hong Kong-Zhuhai: Daraja refu zaidi duniani lafunguliwa rasmi, mambo muhimu kulihusu

Rais wa China Xi Jinping amefungua rasmi daraja refu zaidi duniani, ambalo limekuwa likijengwa kwa miaka tisa. Daraja hilo, ukijumuisha pia barabara zinazolinganisha pamoja, lina urefu wa 55km (maili 34) ana linaunganisha Hong Kong na Macau na jiji la China bara la Zhuhai. Ujenzi wa daraja hilo umegharimu $20bn (£15.3bn) na umecheleweshwa mara kadha. Kwa kulinganisha, gharama hiyo ni zaidi ya bajeti ya mwaka huu ya Tanzania ambayo ilikuwa $14.2 bilioni, hata ukaongeza bajeti ya Rwanda ambayo ni $2.7 bilioni haufikii hizo $20bn. Bajeti ya Kenya mwaka huu ni $30.3 bilioni. Ukatumia mwendo wa kawaida wa kutembea wa 5km kwa saa, basi itakuchukua saa 11 kulivuka daraja hilo ukaamua kutembea. Ujenzi wake ulikumbwa na wasiwasi mara kadha kuhusu usalama wake. Maafisa wanasema watu zaidi ya 18 walifariki wakati wa kujengwa kwa daraja hilo. Rais Xi alihudhuria sherehe ya kuzindua daraja hilo ambayo imefanyika jijini Zhuhai, akiwa pamoja na viongozi wa Hong Kong na Macau. Magari...

Sahle-Work Zewde: Rais mpya wa Ethiopia asiye na 'meno'

Taarifa za Ethiopia kumchagua rais wa kwanza mwanamke zimepokelewa kwa shangwe kote barani Afrika, lakini swali ni; rais huyo ana mamlaka gani? Katika Jamuhuri nyingi duniani cheo cha rais kinashikilia mamlaka yote ya kisiasa na kidola. Jina la rais linawakilisha nguvu na uwezo wa kufanya maamuzi ya mwisho kwa mujibu wa katiba. Changamoto kubwa ya kisiasa duniani na hususan Afrika ni kuwaamini na kuwachagua wanawake katika nafasi kuu za kiuongozi. Na pale inapotokea mwanamke kuchaguliwa katika ofisi kuu ya nchi moja bara zima hushangilia na kupigia mfano. Kuchaguliwa Bi Sahle-Work Zewde na wabunge kuwa rais wa Ethiopia ni habari nzuri katika harakati za kuwainua wanawake wa Afrika, lakini wengi walioshangilia ushindi wake nje ya Ethiopia hawafahamu ukomo wa mamlaka yake.Wengi wanamjumuisha Bi Zewde katika fungu moja na Bi Ellen Johnson Sirleaf, rais mstaafu wa Liberia na Bi Joyce Banda rais mstaafu wa Malawi. Ingawa wote wanabeba jina la Rais, kimamlaka Bi Zewde hayup...

Majambazi wa Ubelgiji waliambiwa warudi tena - na waliporudi wakatiwa mbaroni

Genge la majambazi liliingia katika duka moja kwa nia ya kutaka kuiba. Mwenye duka akawaambia warudi tena baadaye atakapokua na pesa zaidi, na majambazi hao wakaitikia mwito... Ni tukio ambalo unaweza ukalichukulia kama mzaha, lakini kwa mwenye duka mbelgiji anayeendesha biashara ya kuuza sigara mtandaoni ni tukio la kweli na la kuogofya. Watu sita waliingia katika duka la Didier viungani mwa mji wa Charleroi wakiwa na mpango wa kumuibia. Mfanyibiashara huyo aliwaambia wezi hao kurejea dukani hapo mwisho wa siku, wakati atakapokua na pesa nyingi za kuwapatia. Bila kusita watu hao walirejia kama walivyoagizwa na mwenyeduka badala ya kuwapatia pesa alivyowaahidi wakakamatwa na polisi. Akizungumza na BBC alisema "Ni tukio la kuchekesha,". " Wamepewa jina la majambazi wajinga zaidi nchini Ubelgiji." Mwenye duka huyo anasema alitumia muda wa dakika 14 akijaribu kujenga uhusiano mzuri na wezi hao. Didier anasema kuwa alibishana nao kidogo," "Sikuwa...

Mbwana Ally Samatta: Nyota wa Tanzania amfunga kipa wa Liverpool aliyekumbwa na mkosi Europa League Besiktas v KRC Genk

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally Samatta aliendelea kutikisa ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kwa kufungia klabu yake mabao mawili katika mechi iliyochezwa Alhamisi. Aliisaidia klabu yake ya KRC Genk kuwalaza Besiktas wa Uturuki kwa mabao 4-2. Katika mechi hiyo, langoni alikuwa kipa wa Liverool Loris Karius ambaye anakumbukwa kwa kufanya makosa makubwa na kuchangia Liverpool kushindwa kwenye fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwezi Mei mwaka huu. Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya 23 na kisha akaongeza la pili dakika ya 70 baada ya kupokea mpira kutoka kwa Joakim Maehle nyakati zote mbili. Mabao yote mawili aliyafunga kwa mguu wake wa kulia. Sababu ya Samatta kung’ang’aniwa England Mohamed Salah atuma ujumbe kwa kipa Karius Kipa wa Liverpool Loris Karius ashauriwa ahame Kipa wa Liverpool Loris Karius atishiwa maisha Besiktas walikomboa bao moja dakika ya 74 kupitia Vagner Loveawazisha dakika ya 74, lakini Genk waka...