Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2019

Jinsi mmea uliopandwa na wanaanga wa China ulivyoota mwezini na kukauka

Haki miliki ya picha AFP/CHONGQING UNIVERSITY Mmea uliopandwa na wanaanga wa China mwezini umechukua takriban siku nane kuota. Chombo cha angani Cha china kwa jina Change4 kiliwacha kunyunyuzia maji mbegu hiyo ya pamba kama ilivyopangwa nna Chuo kikuu cha Chongqing ambacho kilitunga jaribio hilo. China ilipata mmea wa kwanza mwezini na kwa nini ni muhimu kuendelea na uchunguzi angani Mmea huo uliota katika chombo ndani ya Change4 ambacho kilitua katika eneo la mbali la ,mwezini mnamo tarehe 3 Januari. Eneo ambalo mmea huo ulikulia usingeweza kuishi katika usiku wa mchana wa Lunar Eclipse. Haki miliki ya picha CNSA Wakati huo wote Ujumbe wote wa China utalazimika kulala na mifumo yao yote italala ili kuhifadhi kawi. Hivyobasi mmea huo haukunyunyuziwa maji na kulazimika kufa , kama ilivyokuwa imepangwa. Majaribio mengine Chombo hicho cha China pia kilibeba mbegu za viazi na arabidopsis, mmea kutoka kwa jamii ya haradali pamoja na matunda na na mayai ya chuchu. Ilitaraj...

Samaki wa Mexico walio na uwezo wa kurekebisha matatizo ya moyo

Haki miliki ya picha BHF Image caption Samaki wa tetra anayeishi katika mito kaskazini mwa Mexico wanaweza kuponya mioyo yao Samaki anayeweza kuurekebisha moyo wake huenda ndio suluhu ya matibabu kwa watu wenye matatizo ya moyo, kwa mujibu wa utafiti. Wanasayansi wanao wachunguza samaki wa Tetra kutoka nchini Mexico wamegundua maeneo matatu ya mfumo wa samaki huyo uliochangia uwezo wake kuunda upya tishu za ndani ya moyo. Jeni moja imeonekana kuwa na jukumu kuu katika mfumo huo. Watafiti wanatumai  utafiti  wao siku moja utafanikisha uponyaji wa misuli ya ndani ya moyo kwa wagonjwa ambao wamewahi kupata mshtuko wa moyo. Maelfu ya watu huishi na matatizo ya moyo baada ya kupata mshtuko wa moyo. Kwasababu binaadamu hawawezi kuunda upya msuli ulioharibika, au kujeruhiwa kwa moyo, na mara nyingi watu hulazimika kuishi na hali hiyo au kuishia kufanyiwa upandikizaji wa moyo. Dalili za samaki kwenye pango Kwa utaifiti huu, uliofadhiliwa na taasisi ya British Heart Foun...

Hoteli ya DusitD2 Nairobi: Washukiwa watano wa shambulio la Dusit wawasilishwa mahakamani wakificha nyuso zao

Washukiwa watano wanaohusishwa na shambulio la Jumanne la hoteli ya Dusit mjini Nairobi wamewasilishwa mahakamani . Watano hao ni pamoja na raia mmoja wa Canada. Mahakama iliruhusu upande wa mashtaka kuwaweka rumande kwa siku 30 huku uchunguzi ukiendelea. Takriban watu 21 waliuawa wakati wapiganaji walipovamia hoteli ya DusitD2 . Wanaume wanne walisimamishwa kizimbani katika mahakama kuu jijini Nairobi huku wakificha nyuso zao. Ni washukiwa wa kwanza kuwasilishwa mahakamani wakihusishwa na shambulio hilo baya katika hoteli ya DusitD2 . Lakini hawakusomewa mashtaka yao. Mkurugenzi wa mashtaka ametaka kupewa muda zaidi ili kufanya uchunguzi alioutaja kuwa mgumu na wa kimataifa. Washukiwa wanne ni raia wa Kenya huku wa tano akiwa raia wa Canada mwenye mizizi ya Kisomali., Mapema maafisa wa polisi waliambia BBC waliwakamata watu saba. Mtu mmoja ambaye alionekana na washukiwa hao kabla ya shambulio anaaminika kuwa miongoni mwa wale waliozuiliwa lakini hakuwasilishwa ma...

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema oparesheni imekamilika

Haki miliki ya picha EPA Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema kuwa oparesheni ya kukabiliana na washukiwa wa ugaidi waliovamia hoteli ya Dusit2 mjini Nairobi imekamilika na kwamba washambuliaji wote ''wameangamizwa''. Watu waliyokuwa wamejihami kwa silaha siku ya Jumanne walivamia jengo la hoteli ya kifahari ya Dusir2 katika eneo la Westlands katika jiji kuu la Nairobi nchini Kenya na kuwaua watu 14. Awali maafisa walitangaza kuwa oparesheni hiyo ilikamilika saa kadhaa baada ya shambulio hilo lakini mlilio ya risasi na milipuko ilisikika mapema alfajiri ya leo (Jumatano) Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabab, limedai kuhusika na shambulio. Haijabainika ni washambuliaji wangapi walihusika na shambulio hilo. Akihutubia taifa kwa moja kwa moja kupitia televisheni kutoka Ikulu, rais Kenyatta amesema kuwa watu 14 waliuawa katika shambulio hilo na wengine 700 kuokolewa kutoka jengo hilo. Shirika la msalaba mwekundu hata hivyo limeripoti kuwa waliyofariki k...