
Aliyekukuwa mwendesha mashtaka wa
cheo cha juu mjini New York, amefichua kwa alifutwa kazi na Rais Donald
Trump baada ya kupokea simu kadha zisizokuwa za kawaida kutoka kw rais
huyo wa Marekani.
Preet Bharara aliambia shirika la ABC wiki hii
kuwa alihisi simu hizo kutoka kwa Rais Trump zilikuwa zimevuka mipaka ya
kawaida inayotenganisha ofisi ya rais na uchunguzi huru wa uhalifu.
Bwan Bharara alisema kuwa alifutwa baada ya kukataa kuchukua simu ya tatu ya Trump.
Ikulu ya white House haikujibu mara moja madai hayoiya bwana Bharara.
Bw Bharara ambaye aliteuliwa na Obama na kuhudumu eneo la
Manhattan, alisema ilionekana kuwa Trumo alijaribui kujenga uhusiano
fulani baada ya wawili hao kukutana mwaka 2016.
"Rais obama hakunipigia simu hata mara moja katika kipindi cha miaka saba unusu," Bw Bharara alisema.
Comments
Post a Comment
Here