Tanzania imepoteza takriban shilingi
za kitanzania trilioni 188 (dola milioni 84 za Marekani ) katika
kipindi cha miaka 19 kati ya mwaka 1998 na mwaka 2017 kupitia
usafirishaji wamakinikia ya dhahabu na shaba.
Hii ni kwa mujibu wa Ripoti ya Tume iliyoundwa mwezi March mwaka huu na Rais John Magufuli.Ripoti hii imekuja siku chache baada ya Ripoti ya kwanza iliyojikita kueleza kiasi cha madini na fedha ambazo Tanzania hupoteza kutokana na usafirishaji wa mchanga wenye madini.
Kamati hii ya sasa iliundwa na wataalam wa masuala ya uchumi na wanasheria ambao walikuwa na jukumu la kutazama mikataba ya madini na athari za kiuchumi kwa Tanzania.
Katika Ripoti ya Jumatatu, Tume imedai kuwa Kampuni ya madini yenye makazi yake nchini Canada, Acacia ambayo ni kampuni kubwa zaidi ya madini haikuwahi kusajiliwa nchini humo, hivyo imekuwa ikifanya kazi kinyume cha sheria.
Comments
Post a Comment
Here