Ni kitu cha kwanza wengi wetu
tunakitazama asubuhi na kitu cha mwisho kukiangalia usiku.Simu zetu
haziko mbali nasi na tunaziangalia kila baada ya dakika 12, kwa mujibu
wa mamlaka ya kudhibiti mawasiliano nchini Uingereza, Ofcom.
Ni
mahusiano ambayo yanaonekana kuwa yatadumu zaidi, hivyo tunakudokeza
sheria tano za matumizi ya simu ambayo yanapaswa kutazamwa kwa umakini.1.Kuzungumza na simu wakati wa kula chakula
Watu wengi hufanya hivyo, na zaidi ya 26% ya vijana wanakubali suala hili
''Simu zinapaswa kuwa zimezimwa saa zote wakati wa chakula, mikutano na sherehe,''anasisitiza Diana Mather, mshauri wa masuala ya tabia.
''Mtu uliyenaye ni mtu aliye muhimu zaidi.Hakuna miongoni mwetu asiye na umuhimu.
Hata kutazama televisheni inakuwa imezimwa kwa baadhi ya watu wakati mkiwa kwenye meza ya chakula
Zaidi ya watu wanne kati ya watano walio na umri wa miaka 55 na zaidi wanafikiri haikubaliki kutazama ujumbe wa simu ukilinganisha na 46% ya umri wa miaka 18 mpaka 34.
2. Kusikiliza muziki wenye sauti kubwa kwenye usafiri wa Umma
Kitaalamu
huitwa sodcasting yaani tabia ya kusikiliza muziki kutoka kwenye simu
au vifaa vingine kwa sauti kubwa bila kujali wanaokuzunguka.Inahusisha kutazama video au kucheza michezo ya kwenye simu kwa sauti kubwa.
76% kati yetu tunalipinga lakini hatuachi tabia hiyo.
maceeeeeeeeeeeeen
ReplyDeletetisha saana jembe lang
ReplyDelete