Polisi katika mji wa Zurich nchini
Uswisi wanawashauri watu kuwanunulia mbwa wao viatu ili kuwakinga
kutokana na athari za viwango wa juu vya joto.
Kulingana na kituo
cha habari cha kitaifa SRF, polisi mjini Zurich wamezindua kampeni ya
kuwapa ushauri wafugaji wa mbwa, jinsi wanaweza kuwakinga kutokana na
joto la juu, kutokana na sababu kuwa veranda na barabara zinaweza kuwa
zenye joto.Kiwango cha juu sana cha joto kimeshuhudiwa msimu wa sasa wa joto barani Ulaya, huku Uswizi ikishuhudia kiwango cha juu zaidi cha joto tangu mwaka 1864.
Kiwango cha joto mwezi Julai kilifikia nyuzi 30.
Kulingana na msemaji wa polisi Michael Walker, nyuzi 30 ni sawa na kati ya nyuzi 50-55 ardhini au kwenye lamu kutokana na hali kwamba ardhi huhifadhi joto.
Comments
Post a Comment
Here