Skip to main content

Lionel Messi akutana na kijana aliyevalia jezi ya karatasi Afghanistan

 
Murtaza akiwa na jezi aliyotumiwa na MessiMvulana kutoka nchini Afghanistan aliyepata umaarufu sana mtandaoni alipopigwa picha akiwa amevalia karatasi kama jezi ya Lionel Messi mechi amefanikiwa kukutana na shujaa huyo wake.
Picha ya Murtaza Ahmadi, mwenye miaka sita, akiwa amevalia karatasi hiyo iliyoandika nambari ya jezi ya Messi pamoja na jina lake ilivuma sana mwezi Januari mtandaoni.
Mwishowe, alipokea jezi halisi kutoka kwa mshambuliaji huyo wa Barcelona, ambayo pia ilikuwa imetiwa saini na mchezjai huyo.
Sasa, wawili hao wamekutana ana kwa ana mjini Doha, kwa mujibu wa kamati andalizi ya Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.
Barcelona wamo nchini Qatar kucheza mechi ya kirafiki na Al Ahli Jumanne.
Ahmadi anatarajiwa kutembea kuingia uwanjani akiandamana na Messi.
"Ni picha ambayo ulimwengu ulitaka kuona," aliandika mkuu wa kamati hiyo Jumanne.
"Mvulana wa miaka sita akikutana na shujaa wake, #Messi, ndoto yake ikitimia."
Ahmadi, ambaye anatoka wilaya ya Jaghori, katika mkoa wa Ghazni mashariki mwa Afghanistan, alilazimika kukimbilia nchi jirani ya Pakistan mwezi Mei.
Murtaza alitambuliwa kama mvulana ambaye picha yake ilikuwa ikisambazwa mtandaoni baada ya mjomba wake Azim Ahmadi, raia wa Afghanistan anayeishi Australia, kuwaunganisha waandishi wa BBC Trending na nduguye, Arif - babake shabiki huyo mkubwa wa Messi.

Comments

Popular posts from this blog

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Mwanza: Kibao kipya cha nyota Rayvanny na Diamond Platnumz chafungiwa na Basata

Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.