Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...
BLESSED TO BLESS OTHERS
Comments
Post a Comment
Here