Skip to main content

Posts

Showing posts from 2020

Fahamu ukweli wa dhana tano kuu kuhusu nyoka na maadhimisho ya nyoka duniani

Huku Tarehe 16 mwezi Juni ikiwa ni siku ya maadhimisho ya siku ya nyoka duniani mnyama huyo hutazamwa kwa hatari kubwa, waerevu na mara nyingine hata kuhusishwa na imani potofu na uchawi katika baadhi ya jamii za Kiafrika. Kwa kawaida nyoka anakuwa juu ya orodha ya mambo ambayo mtu anaogopa maishani mwake. Maelfu ya watu duniani hufariki kutokana na sumu kali ya nyoka baada ya kuumwa kila mwaka kwa mujibu wa shirika la afya duniani. Ukosefu wa matibabu na hata matibabu mabaya hufanya vifo hivyo kutokingika. Uso kwa uso na nyoka hatari Nyoka mwenye macho matatu agunduliwa Kasisi aliyewalisha watu nyoka Afrika Kusini, afika Nigeria Sumu ya nyoka ni dawa ya kumaliza uchungu Kuumwa na nyoka huenda kusionekane kuwa janga baya la kiafya. Lakini katika maeneo mengine duniani ni hatari kila siku na huenda kukasababisha maafa ama hata kubadilisha maisha ya mtu. Pengine ndio sababu ya kuwepo dhana tofuati, baadhi potofu, kuhusu wanyama hawa. Hebu tuwafahamu zaidi. CHANZO CHA PICHA, GETTY IMAGES ...

Yusaku Maezawa: Bilionea wa Japan anayetafuta mpenzi wa kuandamana naye mwezini

Yusaku Maezawa anajiandaa kuwa raia wa kwanza atakayesafiri mwezini kwa kutumia chombo cha Elon Musk Bilionea wa Japan Yusaku Maezawa anamtafuta mwanamke atakayekuwa "mpenzi wa maisha" ili aandamane naye kutalii anga za mbali hadi mwezini. Mwanamitindo huyo wa miaka 44, anajiandaa kuwa abiri wa kwanza kwenda mwezini kwa kutumia roketi maalumu inayofahamika kama ''Starship''. Safari hiyo iliyopangiwa kufanyika mwaka 2023, itakuwa ya kwanza kwa binadamu kwenda mwezini tangu mwaka 1972. Katika ombi la mtandaoni, Bw. Maezawa anasema kuwa anataka kufurahia safari hiyo na mwanamke wa kipekee. Mfanyibiashara huyo ambaye hivi karibuni aliachana na mpenzi wake muigizaji Ayame Goriki mwenye umri wa miaka 27, ametoa wito kwa wanawake kuwasilisha maombi yao kuhusu"safari hiyo ya kipekee" katika tuvuti yake. "Japo hisia ya upweke imeanza kunizonga, nafikiria kitu kimoja: kuendelea kumpenda mpenzi wangu," Bwana Maezawa aliandika ka...

VYAKULA 10 VINAVYOFAA KWA WANAUME.

1. Chokolate, hurekebisha mzunguko wa damu na kuondoa mafuta ambayo hayafai kwenye mishipa ya damu hivyo kukuepusha na shinikizo la damu. Ila kula mara kwa mara itasababisha kuongezeka uzito. 2. Samaki kutoka baharini, asa wenye magamba ambao huwa na virutubisho vya zinc vinavyosaidia kuimarisha misuli, moyo na utoaji wa mbegu za kiume. Pia vyakula kama karanga, nyama ya ng’ombe na kuku huwa na kiasi kikubwa cha madini haya. 3. Parachichi, tunda ili huwa na mafuta mazuri ambayo husaidia kuondoa mafuta yenye athari katika mishipa ya damu na hivyo kuzuia magonjwa ya moyo. 4. Tangawizi, kutafuna tangawizi mara kwa mara hupunguza maumivu ya misuli yanayotokana na kufanya kazi nzito au kuumia. 5. Maziwa, huwa na kiasi kikubwa cha protein na potassium ambayo husaidia kujenga  misuli imara. Pia ina bacteria rafiki wanaosaidia kulinda mfumo wa chakula na kuzuia vidonda vya tumbo. 6. Ndizi mbivu, Ina virutubisho vya potassium ambavyo uimarisha misuli, mifupa na kupunguza ...

Papa Francis akiri kukosa uvumilivu kitendo chake cha kumchapa kibao muumini usiku wa mwaka mpya

Papa Francis ameomba radhi kwa kitendo chake cha kumchapa kibao, mmoja wa waumini kwenye kanisa la St Peter's Square huko Rome. Papa alikuwa akisalimiana na watoto na mahujaji na wakati akigeuka mwanamke mmoja aliyekuwa kwenye umati wa watu waliokuwa karibu aliuvuta mkono wa Papa kwa nguvu karibu amuangushe. Hali iliyomfanya Papa kugeuka na kumpiga makofi mawili mkononi mwanamke huyo kwa hasira.                  Badaye Papa alikiri kwamba alishindwa kujizuia na yeye pia huwa anakosea kama binadamu wengine. Hivyo anaomba radhi kwa kitendo hicho kwa muumini huyo na kila mtu. Kitendo cha Papa cha kumzaba makofi ya mkononi mwanamke huyo, kimezua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, hasa Twitter, wengi waki...