Ujumbe wa mahaba wa Reginald Abraham Mengi kwa mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe-Mengi kabla ya kifo chake
Marehemu Reginald Abraham Mengi, ambaye ni bilionea na mfanyibiashara mkubwa nchini Tanzanian alichapisha ujumbe wa mahaba kwa mkewe Jacqueline Ntuyabaliwe-Mengi katika mtandao wa Twitter akimuelezea jinsi anavyompenda.
Katika ujumbe huo wa kuadhimisha miaka minne tangu wawili hao wafunge ndoa yao mwaka 2015, bilionea huyo alisema: Ni furaha kuadhimisha ndoa yetu mpenzi wangu. Imekuwa safari iliojawa na mapenzi na furaha. nakupenda sana, aliandika bilionea huyo.
Ujumbe huo ulimfurahisha mkewe aliyewahi kuwa malkia wa urembo wa Tanzania na ambaye aliujibu kwa kumhakikishia mapenzi tele: Wewe ndio mwanamume wa pekee ambaye ningependelea kuishi maisha yangu nawe , mtu ambaye amekuwa rafiki yangu mkubwa , mwamba wangu, mshauri wangu, na mtu ninayejivunia ,tufurahie siku ya ndoa yetu, nakupenda mpenzi. Ahsante kwa kunionyesha jinsi mtu anavyohisi anapopendwa , aliandika bi Jacquilin.
Ujumbe huo wa mapenzi kutoka kwa bilionea huyo uliwafurahisha watumiaji wa mtandao wa twitter ambao hawakusita kumuliza maswali.
Abdul Zackabul aliandika: Kwa hivyo mzee ulikataa kabisa kutufundisha mapenzi.
Mwengine kwa jina New farias aliandika : Mzee katuzidi kwa pesa mpaka maneno yake pia matamu.
Naye Bwana Venance aliuliza iwapo ni yeye aliendaka ujumbe huo katika mtandao wa Twitter.
Wakati walipokwenda Ulaya kwa ziara ya kibiashara na tamasha la muziki, Mengi alisema kwamba Klynn alikataa kukutana naye licha ya kumtaka afanye hivyo mara kadhaa.
Hatahivyo alikubali wito wake waliporudi nchini Tanzania miezi kadhaa baadaye.
Alisema kuwa alimuoa kwa sababu alikuwa na tabia za mke mzuri.
''Ananipenda sana, anapika, anaosha nguo zangu kwa kutumia mikono yake na sio mashine. Anaheshimu nafasi yangu kama mwanamume na mumewe. Pia anajua nafasi yake kama mwanamke na mke, alisema Mengi katika mahojiano yake miaka ya nyuma.
Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe
Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania.
Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000).
Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd .
Muziki
Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya tanzania kwa jina the Tanzanites.
Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu.
Mnamo mwaka 2004 alitoa kibao chake 'Nalia kwa Furaha'.
Mwaka 2007 alitoa albamu nyengine kwa jina 'Crazy over You' ambacho kilikuwa kibao cha kwanza cha albamu yake mpya.
Comments
Post a Comment
Here