Skip to main content

Mambo 8 muhimu ya kukusaidia kufaulu katika usaili wa kazi

Mwanamke anayetabasamu katika usaili wa kazi
kijana akiwa kwenye usaili wa kazi
Kupata kazi ya ndoto zako si jambo jepesi, na inawezekana ikawa ni vigumu zaidi kama hujui waajiri wanataka nini kutoka kwako.
Ulimwengu wa wa ajira - kwa kampuni kubwa na ndogo - unabadilika kwa kasi sana.
Lakini kuna eneo moja ambalo ni la muhimu kuzingatiwa kwa kila msaka ajira: usaili wa ana kwa ana.
"Usaili huo ni sehemu kubwa zaidi ya mchakato wa ajira," amesema Jane Tippin, ambaye ni gwiji wa masuala ya rasilimali watu ambaye hutumiwa na kampuni kubwa ya benki nchini Uingereza ya Lloyds

Bi Tippin anaamini kuwa uwezo wako wa kujibu maswali mbele ya mtu ama jopo la watu linaweza kujenga ama kubomoa mustakabali wako wa kupata ajira.
Hivyo, unahitajika kujiandaa kikamilifu kabla ya kuingia kwenye chumba cha usaili wa ana kwa ana.
Zifuatazo ni dondoo muhimu zitakazokusaidia kufaualu usaili huo:

1. Fanya utafiti.

Kijana mjasiriamali anaandika maswala muhimu
Chunga usije kushtukizwa na mawswali ndani ya chuma cha usaili, unaweza kupata tabu kuyajibu.
Kama kampuni au taasisi imekupatia majina ya watu watakaokusaili, jaribu kufanya utafiti wa kujua wao ni akina nani na wanafanya nini.
Pia itafiti kampuni ama taasisi hiyo kwa undani: Ipi ni biashara ama shughuli yao kuu? Nani anaiongoza? Ina umuhimu ama nafasi gani katika fani husika? Na kampuni au taasisi zipi ni washindani wao wa kibiashara.
Yawezekana ukawa unajiuliza utazipata wapi taarifa husika, sehemu nzuri ya kuanzia ni kwenye tovuti ya kampuni ama taasisi.
Chukua dondoo na andaa maswali ya kuuliza mwishoni mwa usaili ili kuwaonesha umefanya utafiti kiasi gani kuwahusu.
Utafiti ndiyo kazi ya muhimu ambayo unaweza kuifanya kabla kuingia kwenye chumba cha usaili, na hakika utaona faida yake.

2. Fanya majaribio.
Mwanamke aliyekaa mbele ya jopo la usaili wa kazi
Mwanamke aliyekaa mbele ya jopo la usaili wa kazi

Baada ya utafiti wa kina andaa maswali ambayo unahisi utaulizwa na fanya majaribio ya kuyajibu.
Na endapo utakuwa na shida yeyote ile, rudi mtandaoni. Kuna tovuti kadha wa kadha ambazo hutoa maswali muhimu ambayo huulizwa kwenye chumba cha usaili kwa fani mbalimbali.
Uandaapo majibu yako, fikiria katika muundo wa kujieleza ulio na mtiririko bora. Andaa mifano hai ya namna gani umefanikisha ama unaweza fanikisha yae yote ambayo yanatakiwa katika nafasi ya ajira uliyoomba.
Hadithi fupi fupi za namna gani ulifaulu awali kwenye ajira zako nyengine na uzoefu wako inabidi zioneshe ni kwa namna gani utafaidisha kampuni inayokusaili endapo watakupa ajira.

3. Vaa uvutie.


Kijana aliyevalia vizuri tayari kwa usaili wa kazi
Kijana aliyevalia nadhifu tayari kwa usaili wa kazi
Muonekano wa awali una nguvu kubwa sana. Baadhi ya waajiri hufanya maamuzi ndani ya sekunde 30 za mwanzo za kukutana na mtahiniwa wa usaili.
Unaweza ukawa na majibu mazuri ya maswali, lakini kama mavazi na haiba yako haikuwapendeza watahini wako, utakuwa unapigana katika pambano ambalo lazima ushindwe.
Virginia Eastman, ambaye ni mtaalamu mstaafu wa kutahini watu kwenye usaili anamuelezea bwana mmoja ambaye alimsaili kwa nafasi ya kuongoza kampuni ya habari.
"Harufu yake mbayailitangulia chumbani dakika tatu kabla yeye mwenyewe kuingia. Alikuwa amevaa hovyo: soksi zimechakaa, chakula kimenasia kwenye ukosi wa koti lake...yaani ilikuwa ni moja ya vitu vya ovyo kabisa ambavyo nimewahi kuvishuhudia."
Bila kuuliza, bwana huyo aliikosa ajira aliyoomba.
Japo kampuni inaweza kuwa na sera ya mavazi ya kawaida, hawatakutegemea uende kwenye usaili ukiwa umevalia suaruali ya jeans. Wataalammu wa rasilimali watu wanashauri uvae suti.
Iwapo usaili si wa kazi rasmi, basi inashauriwa uvae shati jeupe na suruari au sketi.
Hakikisha muonekano wako ni nadhifu. Piga pasi siku moja kabla, na hakikisha hauli chakula cha michuzi au rangi rangi kabla ya kuingia kwenye usaili.

4. Salimia kwa kujiamini


Meneja akisalimiana na mwanamume anayetafuta ajira
Meneja akisalimiana na mwanamume anayetafuta ajira

Hiki ni kitu ambacho wengi hukisahau lakini ni muhimu sana.
Mwajiri wako anaweza kukupunguzia alama kwa namna utakavyosalimia uingiapo chumba cha usaili.
Kama unasailiwa na mtu mmoja au unashauriwa uwape mkono huku ukiwaangalia machoni.
Salamu imara inaashiria kuwa unajiamini, unajua ukifanyacho na ni mweledi.
Lakini, chunga usijiamini kupitiliza, utaonekana kuwa ni mkorofi. Ila usipojiamini napo utaonekana kuwa ni muoga.
Pia hakikisha una kitambaa mfukoni, futa jasho kwenye viganja kabla ya kutoa salamu. Hakuna mtu anayependa kupewa mkono wenye jasho.
Na unapokuwa ndani ya chumba cha usaili hakikisha unawaangalia machoni , kuangalia chini ni dalili ya woga.

5. Tabasamu!

Kijana anayetabasamu
Kijana anayetabasamu
Hili ni jambo jepesi kulitaja kuliko kulitenda hususani pale moyo wako unapokuwa unaenda puta, tumbo lako limevurugika na unaweza hata kusahau jina lako.
Hata hivyo, tabasamu ni lugha ya kimataifa ya kusema: "Nina furaha kuwa hapa, mimi ni mtu mwema."
Hivyo basi tandaza tabasamu kubwa unapoingia kwenye chumba cha usaili. Usiliangushe tabasamu hilo wakati wote wa usaili. Ni njia bora ya kupata alama.
Hata hivyo, chunga mikao yako, usijilegeze kwenye kiti, kaa kikakamavu.

6. Usikubali woga ukakutawala
Kundi la wafanyabiashara waliokaa wakisubiri kufanyiwa usali wa kazi
Kundi la wafanyabiashara waliokaa wakisubiri kufanyiwa usali wa kazi

Ukiruhusu uoga ukutawale, kinachofuata kinaweza kuwa... balaa kubwa.
Uoga unaweza kufanya ukasahau kila kitu kwenye utafiti ulioufanya awali, unaweza ukafanya mikono yako ikawa inatetemeka na kutokwa na jasho.
Uoga pia unaweza ukakufanya kushindwa hata kutabasamu.
Kama unajua woga unaweza kukuathiri, basi jaribu kuvuta pumzi na kusema na moyo wako kuwa unaweza, na ndio maana umeitwa kwenye usaili.
Wataalamu wanasema kuwa, endapo utaweza kuushinda woga, basi yawezekana ukapata ujasir wa hali ya juu na kufaulu usaili wako.

7. Kuwa mchangamfu
Msichana mdogo katika usaili wa kazi
Msichana mdogo katika usaili wa kazi

Kabla ya kuketi kwenye kiti cha usaili, tafakari "kipi kinakufanya uwe wa tofauti?"
Ukishajiuliza hivyo, usisite kuwa mchangamfu na kuonesha haiba yako, waoneshe kuwa wewe unastahili. Kumbuka si peke yako uliyeomba kazi hiyo na kuitwa kwenye usaili.
Usisahau pia kusema mambo mazuri kuhusu kazi uliyoiomba - na unapofikia mwisho wa usaili kumbuka kuisifia kampuni na vipi itakuwa fahari kwako kupata kazi hiyo.
Kumbuka uchangamfu na haiba yako ndiyo vitu pekee ambavyo vinaweza kukutofautisha na wengine.

8. Usikate tamaa njiani

Mwanamke akifanyiwa mahojiano
Mwanamke akifanyiwa mahojiano

Hata kama mambo yamekuwa mazito kiasi gani katika chumba cha usaili, usikate tamaa.
Kuna kipindi maswali yanakuwa magumu kiasi kwamba unaweza kudhani kuwa basi na kazi yenyewe ushaikosa.
Usifanye kosa la uamini kitu hicho, jitahidi, pambana mpaka dakika ya mwisho, yawezekana wewe ndiyo umefanya vizuri kuliko mtu yeyote katika usaili huo.
Pia yawezekana swali linalofuatia ndilo ambalo unalimudu kuliko yote yaliyopita.
Ni muhimu kujituliza kifikra mambo yanapokuwa magumu. Una nguvu kubwa ndani yako.
Fanyia kazi dondoo hizi, utaona matokeo!

Comments

Popular posts from this blog

Kiongozi wa Republican ahofia uongozi wa Trump

Kiongozi mmoja wa chama cha Republican nchini Marekani amesema kuwa anahofia maisha ya wajukuu wake saba ,chini ya uongozi wa rais mteule wa Marekani Donald Trump. Christine Todd Whitman ,ambaye ndio mkuu wa shirika la kulinda mazingira nchini Marekani amemshtumu Donad Trump kwa kupuuza ripoti za sayansi. Na amenonya kwamba tishio lake la kuondoa sera za kulinda hali ya anga linaweka siku za usoni hatarini. Wafuasi wa Trump wanasema kuwa sheria za hali ya anga na kawi zinaharabu biashara. Lakini Bi Todd Whitman amesema kuwa Marekani inapaswa kutafuta njia za kukuza biashara bila kuharibu mazingira. Maelezo kuhusu sera za mazingira za bw Trump hayajulikani ,lakini wanaomzunguka wanasema kuwa analenga kuimarisha mkaa, kufungua mabomba mapya ya mafuta, na kuruhusu uchimbaji madini msituni mbalii na kuchimba mafuta katika eneo la Arctic. Kisiasa ,wamependekeza kujiondoa katika makubaliano ya hali ya anga, kufutilia mbali sera ya rais Obama ya kupata kawi safi mbali na k...

Wasifu wa Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi au K-Lynn

Haki miliki ya picha JACQUELINE NTUYABALIWE  Jacqueline Ntuyabaliwe (Jacqueline Ntuyabaliwe Mengi) ambaye pia anajulikana kama K-Lyn alizaliwa tarehe 6 mwezi Disemba 1978 mjini Dar es Salaam, Tanzania. Ni Mwanamuziki , mfanyabiashara na aliwahi kushinda taji la malkia wa Urembo nchini Tanzania (2000). Ni Mwanzilishi wa kampuni ya samani ilioshinda tuzo Amorette Ltd . Babake alitoka kutoka eneo la Kigoma akiwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake huku mamake akiwa nesi. Alisomea elimu yake ya msingi katika shule ya bweni ya Nyakahoja Primary mjini Mwanza kabla ya kuelekea mjini Dar es Salaam ambapo aliendelea na elimu yake ya msingi katika shule ya Forodhani. Jackline ni msichana wa mwisho katika familia ya watoto watatu wa kike Katika utoto wake alikuwa msichana mwenye haya jingi lakini alipendelea sana kusoma vitabu Muziki Alianza usanii 1997 akishirikiana na bendi ya Tanzania kwa jina the Tanzanites. Aliimba kama mmojawapo wa viongozi kwa miaka mitatu. ...

Wafungwa wa Guantanamo Bay wawasili Saudi Arabia

Kundi la wafungwa wa Yemen waliozuiliwa nchini Marekani katika Gereza la Guantanamo Bay wamewasili nchini Saudi Arabia. Waandishi kutoka katika shirika la habari la AFP wamesema watu watatu wameonekana wakipokelewa na familia zao katika uwanja wa ndege ambao kwa kawaida hupokea viongozi Mashuhuri katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Riyadh. Kuhamishwa kwa wafungwa kumetokea siku mbili baada ya Ikulu ya Marekani kuahidi kuendelea na mpango wake wa kuhamisha wafungwa kutoka kataka Gereza la Guantanamo Bay, wakipinga suala ambalo limekuwa likipingwa vikali na Rais mteule wa Marekani Donald Trump.