Kibao kipya kiitwacho, Mwanza, kilichotolewa na wasanii mashuhuri Tanzania Rayvanny na Diamond Platnumz kimepigwa marufuku na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata). Katika taarifa kwa umma iliyotolewa leo Novemba 12 Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza, sababu kuu ya kufungiwa wimbo huo ni ukiukwaji mkubwa wa maadili ya Kitanzania kwa "kutumia maneno yanayohamasisha ngono." Basata pia imeonya vyombo vya habari, na watu binafsi kutoutumia, kuucheza ama kuusambaza wimbo huo kwa namna yoyote ile. "Baraza linatoa onyo kali kwa msanii Rayvanny, Diamond Platnumz pamoja na uongozi wa Wasafi Limited kufuata sheria, kanuni na taratibu wakati wa kuandaa kazi za sanaa. Aidha Baraza limesikitishwa na kitendo hiki ambacho kimefanywa kwa makusudi," imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mngereza. Wimbo huo wa Mwanza ulitolewa rasmi jana na tayari ulishavutia maelfu ya watazamaji kwenye mitandao ya kijamii. Wasanii hao wametakiwa kufuta kibao hiko katika kurasa...
BLESSED TO BLESS OTHERS